Kulia ni Mwl.Chacha Heche ambae ni Katibu wa Chadema Mkoani Mara akiongea na wanahabari nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
Na:George Binagi.
MAHAKA kuu Kanda ya Mwanza jana imeitupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Novemba
25 mwaka jana, katika Jimbo la Tarime Vijijini Mkoani Mara, iliyofunguliwa na
aliekuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM
Christopher Ryoba Kangoye.
Katika kesi hiyo,
wajibu maombi walikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mhe.John Heche
(Chadema), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime pamoja na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali ambapo mtoa maombi alikuwa akiiomba Mahakama kutengua matokeo
ya Uchaguzi Mkuu katika Jimbo hilo kwa kuwa haukuwa huru na haki.
Baada ya Mahakama
hiyo kupitia kwa Jaji Lameck Mlacha kusikiliza utetezi wa pande zote, iliamua
kuifuta kesi hiyo ambayo ilikuwa ni nambari nne ya mwaka 2015 kutokana na hoja
za mleta maombi kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo kutoainisha majina ya
waliokuwa wakilalamikiwa kuvuruga uchaguzi Jimboni humo.
Wakili wa mleta
maombi Costantine Mutalemwa pamoja na Wakili wa mjibu maombi Paul Kipeja
aliekuwa akisaidiana na Wakili Tundu Lisu katika kesi hiyo, wameelezea kuridhika na maamuzi ya Mahakama hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...