Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kupitia Tasinia ya Urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers waingia Zanzibar. Wataalamu kutoka Taasisi ya Manjano Foundation wataendesha mafunzo kuanzia tarehe  1 February 2016 kwenye ukumbi wa  Mtoni Marine Hotel Zanzibar. 
Wanawake 30 wa Zanzibar watanufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Wanawake wakazi wa Zanzibar wanaopenda kunufaika na mradi huo  wanaombwa kwenda kwa usaili na kujiandikisha siku ya Jumamosi tarehe 30 January 2016 kuanzia saa tatu asubuhi kwenye hoteli ya Mtoni Marine mjini Zanzibar.
Mafunzo yana lengo la  kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha, muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. 

Awamu ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa mikopo bila riba kwajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea .
Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 759413234

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...