WAKAZI wa Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, wametakiwa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ili waweze kupatiwa matibabu kwa kuchangia sh10,000 na kupatiwa matibabu mwaka mzima kwa kaya yenye watu sita.
Akizungumza kwenye kijiji cha Engusero wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa kaya kujiunga na CHF, mkuu wa wilaya hiyo Kanali Samuel Nzoka alisema kaya nyingi zikijiunga ndiyo upatikanaji wa dawa unakuwepo.
Kanali Nzoka alisema tatizo la ukosefu wa dawa kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitalini litamalizika, endapo kaya nyingi zikijiunga na CHF kwani serikali nayo itaweka mkono wake ili kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa.
Wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo Kanali Nzoka alijitolea sh20,000 kwa ajili ya kuzilipia kaya mbili za watu 12 wa kijiji cha Engusero na Dosidosi na kuungwa mkono na viongozi wanne wa wilaya hiyo waliojitolea sh10,000 kwa kila mmoja.
Kwa upande wake, Ofisa uratibu na matokeo wa CHF, Nicholaus Mwangomo alisema kila kaya wilayani humo inapaswa kuchangia sh10,000 za gharama za matibabu ili watibiwe kwa kadi na kuachana na mtindo wa kutibiwa kwa fedha.
“Kaya moja ikilipa sh10,00 inapatiwa matibabu kwa mwaka na isipougua inakuwa imewachangia wenzao watakaougua, kwani hata kwenye bima za magari na pikipiki wasiopata ajali wanawachangia waliopata majanga,” alisema Mwangomo.
Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) wa mkoa wa Manyara, Isaya Shekifu alisema mwanachama wa CHF atanufaika na huduma zote za afya za msingi na kinga na tiba kwa zahanati, kituo cha afya na hospitali.
Hata hivyo, ili kudhihirisha kauli mbiu ya awamu ya tano ya hapa kazi tu, Shekifu alikabidhi mashuka 170 ya kujifunika wagonjwa ambapo mashuka 20 yalitolewa kwenye zahanati ya Engusero na mashuka 150 kwa hospitali ya wilaya ya Kiteto.
Shekifu alitaja baadhi ya huduma zinazotolewa ni vipimo vya maabara, wagonjwa wa kutwa na kulazwa, upasuaji kulingana na utaratibu uliowekwa na halmashauri husika na wanachama kupata huduma bora ya afya kwa mwaka.
“Pia watapata huduma ya upasuaji kulingana na utaratibu uliowekwa na Halmashauri zinazoendesha mifuko hii zinapata mapato ya tele kwa tele kutoka serikalini ambayo yatatumika kuboresha huduma za afya,” alisema.
Hata hivyo, ili kudhihirisha kauli mbiu ya awamu ya tano ya hapa kazi tu, Shekifu alikabidhi mashuka 170 ya kujifunika wagonjwa ambapo mashuka 20 yalitolewa kwenye zahanati ya Engusero na mashuka 150 kwa hospitali ya wilaya ya Kiteto.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Manyara, Isaya Shekifu akizungumza kwenye Kijiji cha Engusero Wilayani Kiteto, wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa kuchangia mfuko wa afya ya jamii (CHF) ambapo kila kaya yenye watu sita wanachangia sh10,000 na kupatiwa matibabu kwa mwaka mzima.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, Kanali Samuel Nzoka akizungumza kwenye kijiji cha Engusero, wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa kaya kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ambapo katika uzinduzi huo Kanali Nzoka alizichangia kaya mbili za watu 12, shilingi 20,000 ambazo zitapatiwa matibabu kwa mwaka mzima pindi wakiugua.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, Kanali Samuel Nzoka (kulia) akipokea moja kati ya mashuka 170 yaliyotolewa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wa Mkoa huo Isaya Shekifu (kushoto) kwenye uzinduzi wa uhamasishaji wa kaya kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ambapo kwenye wilaya hiyo ulizinduliwa katika kijiji cha Engusero.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...