Mwigizaji bora wa kike wa Komedi Swahiliwood Salma Jabu ‘Nishabebee’ anawashukru wadau wote wa tasnia ya filamu kwa ujumla wake kutokana na mchango wao ambao wamempa kupitia kazi zake ambazo ameshiriki katika kuigiza na kutayarisha filamu zaidi ya 8 chini ya kampuni yake ya Nisha’s Film Productions.

“Nawashukru wote wanahabari jamaa zangu hata wale ambao wamekuwa wakinishauri kupitia njia mbalimbali, kila mtu kwangu ana mchango mkubwa sana naheshimu hilo kwa kila mtu kwa nafasi aliyo nayo na kuhakikisha wanafanya jambo kubwa kwa ajili yangu Asanteni sana na Mungu awabariki,”anasema Nisha.
Aidha msanii huyo ameamua kuanzisha utaratibu wa kutoa taarifa za maendeleo ya kazi yoyote ambayo atakuwa akiifanya na taarifa kuwafikia wapenzi wa filamu nchini nzima na kuwa ndio njia ya wasanii kujenga mahusiano mema na watazamaji wao ambao kuna wanataka kujua maisha ya wasanii ya kawaida nje ya uigizaji lakini si rahisi.

Filamu ya Kiboko kabisa imeingia sokoni siku ya ijumaa ya tarehe 29.January . 2016 na inapatikana nje nzima anaomba kila mwananchi ajenge tabia ya kununua kazi ambazo ni halali na si kazi bandia ambazo zinashusha maisha ya wadau wa filamu.
Nisha ambaye kwa sasa ni kipenzi cha watoto na wapenzi wa komedi anasema kuwa anatamani kumfikia kila mtu kwa kuongea naye ana kwa ana lakini si rahisi waamini kuwa anawajali ni rafiki wa kweli kwa kila raia wa Tanzania kwani anaamini wote ni ndugu zake.

Kwa mwaka huu Nisha amesema kuwa katika sherehe zake muhimu ambazo huzifanya atahakikisha anakula pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, akina mama wajane na watu walio katika shida kubwa kwenye maisha ya kawaida.
Aidha msanii huyo anachukua muda kuwashukru wanahabari kwa kuwataarifu wapenzi wa kazi zake kwani anaamini bila wao wana mchango mkubwa sana hadi alipofika na anaendelea kuwaheshimu na kutoa ushikiano kwao katika kuhabarisha jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...