Raia wa Ujerumani (kulia) ambaye jina lake halikupatikana mara
moja, ametiwa na mbaroni na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kutaka kuitoroka familia yake katika Hoteli ya Cate Dar es Salaam. Raia huyo alikuwa nchini na mkewe mwenye asili ya Afrika katika kipindi cha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Alijaribu kumtoroka mkewe na mtoto (4) na kuwaacha wakidaiwa deni la sh. 315,000 baada ya kile kilichodaiwa kuzuka ugomvi baina yao.
Mtoto wao (4) akisaidiwa kupandishwa katika Gari
Raia wa Ujerumani huyo akitaka kuruka toka katika Gari la Polisi
Mke wa Raia wa Ujerumani wa pili kulia akiwa anaingia katika Gari kuelekea katika Kituo cha Polisi cha Msimbazi Dar es Salaam na wapili kulia ni kaka wa mwanamke wa Raia wa Ujerumani
Wananchi wakifuatilia kwa karibu tukio hilo
Nimeguswa sana na habari hii. Sijui undani wake, lakini kwa vyovyote vile, namsikitikia huyu mtoto. Katika hali kama hizi, watoto ni wahanga moja kwa moja.
ReplyDeleteHeee, mtoto naye anaenda keko!!
ReplyDeleteweh! Mjerumani vipi? umewakimbia ffu-ughaibuni kina ras makunja unakuja kupewa kibano na ffu wa bongo,mkeo na mtoto rudi nao huko huko na kina ras wanakusubiri kwa hamu
ReplyDeleteNamwonea huruma mtoto, yeye ni innocent victim wa ugomvi wa wazazi wake!
ReplyDeleteWazungu jamani tuwe nao makini, ukishuka bongo jiweke sawa pia..wanadharau, inauma zaidi kwa mtoto wake hata hajali. Kisaikolojia kamuharibu sn. Alafu nani kumuambia amshike afande bega, afande nae kasikilizia. Ingekuwa Ujeruman mwafrika angemshika polis mzungu???
ReplyDelete