SERIKALI yaombwa kuchangia chakula cha watoto wakiwa shule ili kuwasaidia kusoma wakiwa wameshiba kwani watoto hawawezi kusoma wakiwa na matumbo hayana chakula.
Hayo yamesemwa na Shule kuu ya Elimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Joviter Katabaro wakati akichangia maada katika mkutano wa kujadili masuala ya elimu katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyrere jijini Dar es Salaam leo.
Nae Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Haki Elimu, John Kalage kuwa wamependekeza Lugha ya Kiswahili na Kiingereza iwe lugha ya kufundishia na kujifunzia kwa ngazi zote ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Pia ametoa wito kwa serikali kuwa kutoa elimumsingi bure sabamba na kupunguza michango ya wazazi mashuleni.
Aidha Karage amesema kuwa ili kuhakikisha ubora mashuleni, shule, taasisi na vyuo vinapaswa kufanyiwa ukaguzi kuhusu ufundishaji na ujifunzania pamoja na mazingira kuwa mazuri.
Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Bashiru Ally akizungumza na wadau wa elimu leo jijini Dar es Salaam wakati wakijadiliana kuhusiana na masuala mbalimbali ya elimu kwa watoto waliotolewa fedha na Serikali kwaajili ya kutolewa elimu bure kwa elimu ya Sekondari na Shule za msingi. Kulia ni Profesa Mshiriki wa chuo kikuu cha Dodoma, Profesa Willy Komba.
Profesa Mshiriki wa chuo kikuu cha Dodoma, Profesa Willy Komba akizungumza na wadau wa Haki elimu leo wakati wa kijadili Lugha gani itumike katika kufundishia kwa wanafunzi wa shule za hapa nchini.ilikwa alisema sema kuwa wanafunzi wasichanganyikiwe kuhusiana na lugha ambayo itatumika kufundishia kwa masomo yao.
Baadhi ya wadau wa elimu wakiwa katika mkutano huo wa kujadili masuala ya elimu uliofanyika jijini Dar es Salaam leo
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...