Mkurugenzi mkuu wa World Lung Foundation(WLF) Dk Nguke Mwakatundu akimkabidhi Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma Mhandisi John Ndunguru moja ya kifaa cha kumsaidia mama mjamzito kuvuta mtoto wakati wa kujifungua.
Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma John Ndunguru akikabidhi moja ya kifaa cha kumsaidia mama mjamzito kujifungua salama kwa kumvuta mtoto kwa uongozi wa hospita ya Mkoa, uliotolewa na shirika la World Lung Foundation.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma John Ndunguru akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada wa vifaa saba vya kumsaidia mama mjazito kujifungua katika hospital ya Mkoa wa Kigoma msaada uliotolewa na shirika la Word Lung Foundation
Na Editha Karlo wa Blog ya Jamii, Kigoma
Shirika lisilo la kiserekali la Word Lung Foundation(WLF) limetoa msaada wa vifaa saba kwaajili ya kumsaidia mama mjamzito wakati akijifungua kumvuta mtoto aliyeshindwa kutoka kwa kutumia ombwe(vacuum extractors) vifaa hizo vimetolewa katika hospital ya Mkoa wa Kigoma.
Akiongea wakati wa kukabidhi msaada huo wa vifaa vya kusaidia akina mama wajawazito kujifungua salama kwa uongozi Serekali ya Mkoa na hospital Mkurugenzi Mkuu wa wa shirika hilo Dk Nguke Mwakatundu alisema Kuwa shirika hilo limekuwa mstari wa mbele kuhakikisha vifo vya akina mama na watoto wachanga vinapungua.
Alisema utumiaji wa vifaa hivyo vya kuvuta watoto inasaidia akina wengi kujifungua bila ya upasuaji jambo linalowapunguzia adha mbalimbali zitokanazo na upasuaji kama vile maumivu, kuuguza kidonda muda mrefu pamoja na matatizo mengine.
Alisema vifaa hivyo vinathamani ya shilingi 30,450,000 ambavyo vitaboresha utoaji wa huduma kwa akina mama wakati wa kujifungua.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Kanali mstaafu Issa Machibya alisema kuwa uongozi wa Mkoa wa Kigoma unalishuru shirika hilo kwa juhudi wanazofanya za kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga katika Mkoa wa Kigoma.
"Kwakweli World Lung Kigoma mnaipenda sana kwani ipo Mikoa mingi hapa nchini yenye matatizo haya lakini nyie mmechagua kuja kufanya kazi kwenye mkoa huu nawapongeza kwa hili"alisema Katibu tawala wa Mkoa
Alisema Mkoa utashirikiana shirika hilo katika kuhakikisha vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga vinapungua Mkoani Kigoma.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa hospital ya Mkoa wa Kigoma maweni Dk Fadhil Kabaya alisema kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja shirika hilo limeweza kushirikiana na vituo vya afya 9 wanavyofanya navyo kazi na kupata mafanikio mbalimbali.
"Akina mama 18281 walijifungulia katika vituo hivyo, akina mama 1613 walifanyiwa upasuaji na akina mama 166 walipatiwa huduma ya kumvuta mtoto kwa kutumia ombwe yaani vacuum extraction, pia vifo vinavyotokana na uzazi vimepungua kutoka 49 mwaka 2014 hadi vifo 38 mwaka 2015 sawa na asilimia 22"alisema Dk Fadhil


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...