
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu serikali kuhamishia akaunti zote za mapato Benki Kuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Hazina wa Benki ya CRDB, Alex Ngusaru na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa (kushoto) akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa (kushoto), Mkurugenzi wa Hazina wa Benki ya CRDB, Alex Ngusaru na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya CRDB, Philip Alfred wakiwa katika mkutano huo.
SIKU
moja baada ya Serikali kutangaza kuchukua hatua za kupunguza riba za
mabenki kwa wananchi kwa kuagiza akaunti za mashirika na taasisi zake
katika mabenki ya kibiashara zifungwe na kuhamisha fedha zilizopo katika
akaunti hizo kwenda Benki Kuu ya Tanzania (BoT), benki ya CRDB imeunga
mkono hatua hiyo.
Pia
benki hiyo imewataka wananchi wasiwe na hofu juu ya mpango huo,
kutokana na hofu iliyojengeka kwamba kuna hatari benki za kibiashara
kufilisika nchini.Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei alisema uamuzi uliofanywa na
Serikali utasaidia kukuza uchumi pamoja na kutambua fedha zake mahali
zilipo.
Alisema
Serikali ina haki na nia njema kwa kutaka akaunti hizo zifunguliwe BoT
kwa kuwa zimekuwa zikifunguliwa kwenye mabenki makubwa ya kibiashara,
huku baadhi ya Wakala wa ukusanyaji wa fedha wakishindwa kuzifikisha
serikali kama inavyotakiwa.
Pia
alieleza kuwa mfumo huo hauna utofauti na awali kwani utofauti
utakuwepo kutokana na mashirika na taasisi kufungua akaunti BoT, ambapo
lengo kubwa ni walaka wa Hazina kulenga kuboresha mapato ya serikali
ammbayo yanaweza kutumiwa kwa namna mbalimbali.
“Mfumo
huu…utakuwa hauna tofauti na ilivyo sasa kwa kuwa fedha zitakazokuwa
zikiingizwa kwenye akaunti hizo ni zile zilizokuwa zikiingizwa kwenye
benki awali, ili kupunguza kiwango cha riba,”alisema.
Pia
alisema hofu nyingine inayojengeka kwa wananchi inatokana na mfumo huo
kutotumiwa kwa muda mrefu na BoT, licha ya kuwa kuna baadhi ya nchi
inatumia mfumo huo na hakuna madhara yoyote.
“Hivyo
tunafikiri maamuzi hayo hayana athari zozote kwani nchi mbalimbali
zimekuwa zikitumia mfumo huo ikiwemo Uganda, Rwanda na Kenya ila kwa
kwetu unaonekana mgeni kutokana na kutotumika kwa muda mrefu,”alisema.
Pia
Dk.Kimei kuwa kutokana na uwepo wa mfumo huo benki za kibiashara
zitawakopesha zaidi sekta binafsi, ikiwa tofauti na malalamiko ya mwanzo
kwamba Serikali inapata manufaa kutokana na kukopeshwa zaidi.
“Hii
itasaidia hata wananchi wa kiwango cha chini kuchukua mikopo kutokana
na riba kuwa ndogo, ambapo hata wananchi wa chini wataweza kuchukua
mkopo, ikiwa tofauti na awali wananchi wanashindwa kuchukua mikopo
kutokana na riba kuonekaa kuwa juu zaidi ya asilimia 10,”alisema.
Mbali
na hilo, pia Kimei alisema endapo riba ikiwa inapungua itasaidia kukuza
uchumi kutokana na wananchi wengi wa hali ya chini kuchukua mikopo.


Ndio maana customer service ya hizi banks ilikuwa imekufa. Sababu walikuwa wanafanya biashara na pesa za Taifa/serikali na kuwa na kiburi cha kutowajali wananchi wenye nchi yao.
ReplyDeleteHii italeta mwamko wa wafanyakazi wa ma-bank kuanza kutafuta masoko kwa wananchi wa kawaida.
Hongera Mh. Rais wa awamu ya tano kwa kuliona hili.
Ni muhimu kwa sekta binafsi kubuni mbinu mpya na uendeshaji wa biashara zao bila kutegemea kubebwa na serikali.
ReplyDeleteAmen
Delete