SHIRKA la ndege la Etihad limepokea tuzo ya heshima katika mabadiliko ya kifedha kwa mwaka 2015 kutoka kwa kampuni ya kimarekani ya Innovation Enterprise inayoongoza kwenye masuala ya uvumbuzi katika sekta uwekezaji.

Tuzo hiyo ilitolewa kwa Shirika la Ndege la Etihad ambalo lilifanikiwa kuzishinda kampuni nyingine kupitia kituo chake cha nje cha mpango wa Mabadiliko ya kifedha. Programu hiyo iliundwa mahususi  kwa ajili ya shughuli za utendaji na uendeshaji wa shirika hilo katika mazingira ya gharama nafuu.

James Rigney, Afisa Mkuu wa fedha wa shirika la ndege la Etihad alisema…”Tunajisikia fahari kupokea tuzo hii kwa kazi kubwa iliyofanywa na Timu yetu ya mipango ya fedha. Tulikuwa na muda mfupi tu wa miezi sita katika kuhakikisha tunatekeleza mabadiliko ya mpango wetu, na juhudi yao kwenye kazi hii ulitufanya tuweze kupunguza nguvu kazi kifedha, kuanza kusonga mbele na muundo wa kikanda uliopunguza gharama na kukuza kipato hadi kufikisha dola za kimarekani milioni 28 kama akiba huku lengo likiwa kufikia dola za kimarekani milioni 50 milioni hadi mwisho wa mwaka huu.”

Awamu ya kwanza ya kituo cha nje cha mpango wa Mabadiliko ya kifedha kilihitaji kuundwa kwa kituo kimoja chenye ubora kitakachoshughulikia miamala yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1 kutoka nchi zaidi ya hamsini. 

Awamu ya pili ilitazamia shirika la ndege la Etihad kupitisha mipango ya kuboresha michakato muhimu na kuondoa vikwazo, ili kuhakikisha shughuli hizo zinafanyika kituoni hapo bila kukiuka viwango vya juu vya kuongoza ndege Shirika la Innovation Enterprise ndio linaongoza katika kukuza ubunifu katika mipango ya fedha na taaluma ya uchambuzi, na ni mratibu mkubwa wa matukio katika sekta ya Mipango ya fedha na uchambuzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...