Leo ni siku ya kuzaliwa ya Saleh Ally, mchambuzi na mwandishi mkongwe wa michezo nchini Tanzania ambaye kwa sasa ni Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi yanayomilikiwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd na Mmiliki wa Blog ya Saleh Jembe.
Saleh Ally amefanya mengi katika ulimwengu wa michezo na burudani ambapo amesharipoti michuano mbalimbali mikubwa ikiwemo Kombe la Dunia na pia amesafiri katika nchi nyingi za mabara tofauti akifanya kazi hiyo.
Kazi zake nyingi nzuri zimekuwa hamasa kwa waandishi wengi ambapo amekuwa kioo ‘role model’ kwa wengi wao. Tunamtakia kila la kheri katika maisha yake yote na Mungu ampe baraka nyingi.
Happy birthday Saleh Ally



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...