Na Bashir
Yakub.
Ni muhimu kujua
tofauti ya kisheria
ya maneno ubatili na
ubatilifu kabla ya kujua
lolote kuhusu hadhi/nafasi
ya kisheria ya ndoa
pasi na tendo la
ndoa. Ujuvi wa
maneno ubatili na
ubatilifu ndio utakaopelekea kufahamika
vyema kwa haya makala.
Kisheria kuna tofauti
kati ya ubatili na
ubatilifu.
1.TOFAUTI YA
KISHERIA KATI YA
UBATILI NA UBATILIFU.
( a ) UBATILI.
Maana ya ubatili
kisheria ni kuwa
jambo hilo haliruhusiwi
kabisa. Halitakiwi kutendwa kwa
namna yoyote ile . Kwa
lugha ya kitaalam matendo
haya huitwa “VOID
ACTS”. Ni matendo haramu
kabisa. Kwa mfano kwenye
ndoa matendo haramu
ni pamoja na
mtu kutangaza ndoa
na mtoto wake
wa kuzaa, au
mtu na mzazi
wake, au kutangaza ndoa
ya jinsia moja
au kutangaza ndoa
na mtu mwenye
umri mdogo. Kwa
namna yoyote matendo
haya ni batili( void), haramu
na hayaruhusiwi kwa
namna yoyote.
( b ) UBATILIFU.
Maana ya
ubatilifu kisheria ni
kuwa tendo linakuwa si
halali wala si
haramu isipokuwa ili
liwe halali au
haramu litategemea uamuzi
wa upande mmoja
kati ya pande
mbili zilizokubaliana.
Upande mmoja unaweza kuamua
jambo liwe halali
au liwe haramu ,
nitatoa mfano.

Mtu akikuuzia
gari ambalo liko
tofauti na ulivyokuwa
umemwagiza katika mkataba
wenu tendo hilo
sio halali wala
sio haramu/batili ila ni batilifu. Hii
ina maana kuwa
ukiamua kulipokea gari
hilo na kulikubali hivyohivyo lilivyo
basi umehalalisha tendo
hilo na limekuwa
halali. Ukikataa kulipokea kwakuwa
linapingana na kile
kilicho kwenye makubaliano
basi tendo hilo la
kuletewa gari lililo tofauti linakuwa
haramu/batili.
Basi ifahamike
kuwa katika sheria
yapo matendo ambayo
si halali wala
si haramu. Na
haya kwa kitaalam
huitwa”voidable acts”. Na hicho
ndicho kitakachoelezwa katika kujibu
swali la nafasi ya kisheria
ya mtu ambaye hawezi
kutekeleza tendo la
ndoa.
2. KUTOWEZA
KUTEKELEZA TENDO LA
NDOA.
Sheria imesema kushindwa
kutekeleza tendo la
ndoa”incapable of consummating”. Maana ya hili
ni kushindwa kabisa
kutekeleza tendo la
ndoa na sio
uwezo mdogo katika
kutekeleza tendo la
ndoa. Tofauti hii ni
lazima ipambanuliwe bayana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...