Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Mary Maziku (kushoto)akisoma taarifa ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Ndugu Kinana anatarajia kukagua na kushiriki miradi mbalimbali ya chama na ushiriki wa wananchi katika kujiletea maendeleo yao.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa CCM mkoa wakisikiliza wakati Kaimu Katibu wa Mkoa Ndugu Mary Maziku akiwakilisha taarifa za maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye ofisi za CCM mkoa wa Singida. 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na kamati ya siasa ya CCM mkoa wa Singida mara baada ya kupokea taarifa za maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi jengo la CCM mkoa wa Singida ikiwa sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.

PICHA NA MICHUZI JR-MMG-SINGIDA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...