Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi limepitisha bajeti ya zaidi ya Sh. 67,613,232,516 Katika kikao maalum cha baraza la Madiwani kwa mwaka 2016/2017 ikiwa ni makisio ya mwaka mpya wa fedha utakaoanza mwezi wa 07 mwaka huu.
Makisio ya bajeti hiyo yamegawanyika katika sehemu kuu tatu, ambazo makusanyo ya ndani yanayokadiliwa kufikia kiasi cha jumla Sh.4,189,145,436 , ruzuku kutoka serikali kuu zaidi ya 44,063,827,880 ambazo ni kwa ajili ya mishahara na matumizi ya kawaida, huku miradi ya maendeleo ikiwa na jumla ya sh.21,294,808,400.
Akiizungumzia bajeti hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Mufindi Bi. SAADA MALUNDE, amebainisha kuwa, Halmashauri imeanzisha vyanzo vipya vya mapato amabapo kuanzia mwaka wa Fedha 2016/2017 Halmashauri inataraji kuanza kutoza kodi za majengo kwa wakazi wake pamoja na tozo ya ushauru wa madini kwa kuzingatia vigezo vitakavyowekwa kwa lengo la kuongeza mapato ya ndani.
“Huwezi kutoza kodi au ushuru wowote pasipo kutoa elimu kwa jamii, baada ya baraza kuridhia, sisi kama watendaji tunajipanga kwenda kutoa welimu kwa umma ambapo, tutaenda kwenye kila kata na kutoa elimu kweye kamati za maendeleo za kata kisha halmashauri za vijiji na hatimaye kwenye mikutano mikuu ya vijiji ili wananchi waweze kufahamu kabla ya kuanza kutoza mapema mwezi wa saba”
Kizungumza wakati akifunga kikao cha baraza hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wiaya Mufindi FESTO MGINA, metoa rai kwa Madiwani na wataalam wa Halmashauri ya Mufindi kuhakikisha kwa pamoja, wanashirikiana katika suala la ukusanyaji wa mapato mara baada ya kuanza kwa mwaka mpya wa Fedha ili Halmashauri iweze kufikia malengo na kutoa huduma kwa jamii.
Aidha, Mgina ametanabaisha kuwa, pamoja na randama ya bajeti hiyo kwa mwaka ujao wa Fedha, Halmashauri imeambatisha maombi maalum kwa sirikali kuu ambayo ni pamoja ombi la shilingi Sh. 550,000,000 kwa ajili ya ukarati wa shule ya Malangali ikiwa ni miongoni mwa shule kongwe hapa nchini ambazo viongozi wengi wa Taifa hili walipata kusoma Sanjari na ombi la kupatiwa magari matatu yenye thamani ya Sh.540,000,000 maalum kwa ajili kusafirishia wagonjwa ambayo yatasambazwa katika vituo vitatu vya afya vilivyopo tarafa za Sadani, Ifwagi na Kasanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...