Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amezindua wiki ya mahakama kwa matembezi mjini Iringa yaliyoongozwa na brass band ya Jeshi la Magereza. Akihutubia majaji pamoja na wananchi amesisitiza uharaka wa kutoa HAKI. kesi nyingi zinachelewa kuisha na wananchi wengi wamedulumiwa haki yao na huu ni uvunjwaji katiba.

Pia amesisitiza wakimama wasimamiwe haki zao. Kasesela pia alisisitiza polisi na ofisi ya mwanasheria mkuu wakae pamoja kubaini kwa nini kesi nyingi ushahidi unakuwa haujakamilika? Wakamilishe ushahidi kabla ya kufungua kesi. Bila haki nchi haiwezi kuendelea hata kidogo.

Akitoa salamu zake Jaji Mfawidhi kanda ya Iringa Mh Mary Shangali aliahidi kuharakisha kesi pia kutembelea magereza yote ili kubaini waliocheleweshewa haki zao.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akiongoza matembezi ya wiki ya Mahakama.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akihutubia wakati wa ufunguzi wa wiki ya Mahakama, uliofanyika jana Mkoani humo.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu mkoa wa Iringa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...