Mpango wa Kijamii wa Uzalishaji Salama ili kusaidia kaya masikini kupambana na umasikini (PSSN) umefanikiwa kuwa na matokeo mazuri kwa kusaidia kaya Milioni 1.1 nchini na kusaidia juhudi za serikali kupambana na umasikini.

Hayo yamefahamika wakati washirika wa maendeleo ambao ni Umoja wa Mataifa, Benki Kuu ya Dunia, Serikali ya Uingereza kupitia kitengo cha Maendeleo ya Kimataifa, Irish Aid, USAID, Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Sweden (SIDA) walipotembelea miradi ya maendeleo katika wilaya za Unguja, Chamwino, Babati, Sumbawanga (Manispaa na Wilaya), Singida na Hanang kwa kipindi cha siku tatu kuanzia Januari, 19 hadi 22.
Bi. Kazijya Kila ambaye ni mmoja wa wanufaikaji wa fedha akitoa ushuhuda kuhusu mradi wake wa chakula ulivyowezeshwa na TASAF ambapo hadi hivi sasa anatengeneza faida ya Shilingi 7000 kwa siku na kabla ya kuwezeshwa alikuwa akikaa nyumbani na mama yake bila kuingiza kipato chochote.

Katika Mpango huo ambao utekelezwaji wake unasimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) unafanyika Tanzania Bara na Tanzania visiwani ukiwa na lengo la kuzisaidia kaya masikini pesa za matumizi ili kukidhi mahitaji ya kupata chakula pamoja na kuwawezesha kusaidia watoto wao kupata elimu jambo ambalo linaonekana kuzaa matunda kwa maeneo mengi ikiwepo Tanzania visiwani.

Serikali ya Tanzania imekuwa ikisaidia na washirika wa maendeleo ili kupunguza umaskini uliokithiri kwa wananchi wake na mwaka 2013 iliweka mpango wa kusaidia kaya masikini 275,000 kwa kipindi cha miaka mitano na tangu ianzishe mpango huo ilifanikiwa kusaidia kaya 275,000 kwa mwaka 2013 pekee katika wilaya nane nchini.
Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi Mohamed (kushoto) na Msimamizi wa mpango wa PSSN, Bw. Ramadhani Madari wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu kwa wanufaikaji wa fedha hizo.

Na mpaka kufikia sasa mpango huo umeshatoa malipo mara 12 na jumla ya kaya masikini milioni 1.1 zimeshafaidika na mpango huo ikiwa ni kwa wilaya 161 na vijiji 9789 nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...