Mtoto wa kiume mwenye uraia wa taifa la Afghanistan ambaye hivi karibuni aligonga vichwa vya mitandao ya kijamii kwa ku vaa fulana ya mfuko wa plastiki ilio na jina la Lionel Messi hatimaye amepata jezi nzuri kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Argentina.

160225110545__88438940_messi_boy

Murtaza wa Afghan akivalia jezi nzuri aliyotumiwa na Messi

BBC ilimsaidia Messi kumtafuta mtoto huyo ambaye anajulikana kuwa shabiki mkubwa wa mchezaji huyo wa Argentina. Murtaza Ahmadi mwenye miaka 5, anatoka katika wilaya ya Jaghori mashariki mwa mkoa wa Ghazni nchini Afghanistan.

Timu ya usimamizi wa Messi ilithibitisha siku ya Alhamisi kwamba Murtaza alitumiwa jezi ya mshambuliaji huyo wa Argentina iliotiwa saini pamoja na mpira kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Barcelona.

“Ninampenda Messi na fulana yangu inasema Messi ananipenda,”Murtaza alisema,tayari akimuigiza mshambuliaji huyo anavyosheherekea bao lake.
Msako wa mtoto huyo katika mtandao ulisababishwa na picha moja iliyoenea katika mitandao ikimuonyesha amevaa fulana ya plastiki ya Messi.

160127133410_afgha_boy_messi_640x360_twitterjoynaw5

Hii ndio jezi aliyotengeza nyumbani na kuvaa

Source: BBC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Alaihi salaam Humma Allah, chonde chonde Taliban msije kumkaba mtoto huyu na kumpora Jezi yake. alex bura dar.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...