NMB imekabidhi madawati 730 yenye thamani ya shilingi milioni 75 kwaajili ya shule za msingi 15 zilizopo wilayani Kiomboi – Singida huku kila shule ikipata madawati 50.
Msaada huo ni moja ya ushiriki wa benki katika maendeleo ya jamii na hivyo kuhakikisha kuwa jamii inayoizunguka benki hiyo inafaidika kutokana na faida wanayoipata. Katika mpango wake, NMB imetenga asilimia moja ya faida inayoipata baada ya kodi ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni 1 kwaajili ya kuchangia maendeleo ya wananchi ikiwemo kusaidia sekta ya afya na elimu.
Shule zilizofaidika na msaada huo ni : Wala, Kisonga, Kigulu, Ujungu, Luzilukulu, Kiomboi, Lulumba, Isui, Tulya, Kitukuta, Mugela, Msai, Masagi, Kinkungu na Mtekente.
Wakati huo huo Nmb
imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya
shilingi million 25 kwa mkuu wa mkoa wa singida.Vifaa tiba hivi vimetolewa
kwaajili ya hospitali ya mkoa wa Singida ili kupunguza uhaba wa vifaa tiba
ambao umekua ukiikumba Hospitali hii. Vitanda, magodoro na mashuka ni miongoni mwa vifaa tiba vilivyo tolewa na
NMB.
Akizungumza wakati wa
makabidhiano Meneja wa Kanda ya Kati NMB
Bw.Stratoni Chilongola alisema “NMB inathamini wateja wake na ndio maana NMB imetenga Zaidi
ya shilingi bilioni 1 kwaajili ya kuchangia maendeleo ya wananchi ikiwemo
kusaidia sekta ya afya na elimu. Kiasi hiki kinatufanya kuwa benki ya kwanza
katika kuchangia maendeleo ya jamii kuliko benki yoyote hapa nchini.”
Hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika katika viwanja vya
hospitali ya mkoa Singida iliwagusa wananchi wengi ambao wameshukuru uwepo wa
tawi NMB Mkoani Singida.
![]() |
| Afisa Elimu wa Wilaya ya Kiomboi Clement Berege (kushoto) akipokea msaada huo |
Wanafunzi wakiwa na madawati hayo
Wanafunzi wakipeleka madawati madarasani





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...