BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imekuwa ikifuatilia kwa makini majadiliano yanayoendelea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kufuatia video iliyotumwa katika YouTube https://www.youtube.com/watch?=iveX49WE7fw na imekuwa ikisambazwa kupitia njia mbalimbali za habari ikimuonesha mtu mmoja kutoka nchi jirani akisema kuwa Olduvai Gorge ambayo kimsingi iko Tanzania kwamba iko Kenya.

Video hii imeibua majadiliano katika mitandao ya kijamii baina ya watanzania na watu wengine ambao wanaitakia mema Tanzania na wanaoelewa vizuri kuwa Olduvai Gorge iko Tanzania.

Bodi ya Utalii Tanzania kama taasisi ya Umma yenye jukumu la kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii imeshtushwa na video hii iliyojaa upotoshwaji mkubwa ambao tunaamini mbali ya malengo mengine inalenga kuchafua kazi nzuri ambayo imekuwa ikifanywa na Bodi kwa kushirikiana na wadau wengine katika kutamgaza vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo Olduvai Gorge.

Tunapenda kuchukua fursa hii kupinga vikali upotoshwaji huu uliofanywa na mtu huyo wakati akihutubia mkutano amabao tumeambiwa ulikuwa ni wa Vijana wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Amerika mwezi Agosti mwaka jana. Tunapenda dunia ifahamu kuwa kama ilivyo kwa Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Zanzibar n.k Olduvai Gorge mahali panapoaminika kuwa ndipo binadamu wa kwanza duniani aliishi na ambako Dr. Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la binadamu huyo wa kale anayesadikiwa kuishi miaka takribani milioni 2 iliyopita iko pia Tanzania na si mahali pengine popote duniani. Eneo hili la Olduvai Gorge liko katika bonde la ufa katikati ya bonde la Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Manyara nchini Tanzania.

Tunatoa wito kwa watanzania mahali popote walipo kuendelea kuunga mkono juhudi za Bodi ya Utalii Tanzania za kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya Utalii kwa kujibu na kusahihisha papo hapo bila woga mara tu taarifa ya upotoshaji kuhusu nchi yetu inapotolewa iwe ni kwenye mikutano ya ndani ya nchi au ya Kimataifa. Tunaamini kuwa ni jukumu la kila mtanzania kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya Utalii badala ya kuiachia TTB kazi hii peke yake. 

Yawezekana katika mkutano huo wa vijana ambao mjumbe huyo wa nchi jirani alipata fursa ya kuzungumza na kufanya upotoshaji huzo, wajumbe wa Tanzania pia walikuwepo ambao wangweza kukosoa upotoshaji huo papo hapo na kuelezea ukweli na usahihi wa mahali ilipo Olduvai Gorge.

Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano
BODI YA UTALII TANZANIA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. ktk huo mkutano hakukua na vijana kutoka TZ?

    ReplyDelete
  2. NDIYO NI JUKUMU LA WATANZANIA TULIOKO NJE KUITANGAZA VYEMA NCHI YETU.....HILO TUNALIFANYA SANA NA WALA HALINA UBISHI. LAKINI PIA NI JUKUMU LA TTB KUFANYA KAZI YAO KWA JUHUDI KUBWA NA MAARIFA SIYO KUNYAMAZA KAMA KONDOO VITU KAMA HIVI VINAPOTOKEA. WATANZANIA TUWE PATRIOTIC LAKINI PIA SERIKALI ITENDE HAKI KWA UPANDE WAKE, HAYA MAMBO TUNAYOYASIKIA YA ITIKADI YA VYAMA HASA CCM INAVYOTUMIA NGUVU PALE INAPOONA INASHINDWA (KAMA PALE KWENYE UCHAGUZI WA MEYA WA DAR, UCHAGUZI WA ZANZIBAR NA MENGINEYO) YANAWAKATISHA TAMAA WATANZANIA WALIO WENGI NA WANAOPENDA HAKI NA HIVYO KUWAFANYA WASIWE NA UPENDO KWA NCHI YAO.

    ReplyDelete
  3. Sawa. Je TTB imewasilian na muandaaji wa mkutano na kurekebisha na kukanusha kauli hiyo potofu. Je TTB imetoa tamko twitter, facebook ambako hiyo kauli potofu imeonekana.Lazima bidii ifanyike kufuta kauli potofu kwa lugha mbali mbali. Aidha muandaaji wa mkutano atoe kauli kwa wahudhuriaji wa mkutano huo kurekebisha na kujitenga na kauli hiyo potofu.

    ReplyDelete
  4. wapumbavu hawa, kazi zao kukaa tuu ofisini wasubirie moto uwake ndio wakimbizane kuuzima. sasa tangu august leo ndio wamejua hilo?????

    ReplyDelete
  5. It is a mark of how well, or otherwise, we have promoted ourselves and world heritage sites in Tanzania, that someone can stand up and utter a blatant falsehood, to an international audience and go unchallenged for the good part of seven months!
    TTB and the Ministry of Foreign Affairs were beaten to challenge this ignorant made on an international platform by a private account on facebook and Jamii Forums on twitter. Who has the better budget to speak in defence of and in the interests of the United Republic of Tanzania?
    Who represented Tanzania at this conference? It is most likely Tanzania was represented but to what effect? With this sort of performance one can understand why JPM banned unnecessary foreign trips.

    ReplyDelete
  6. Hakuna faida ya sisi kukasirika kwani watalii huwa they don't care uko Tanzania au Kenya as long as uko east africa au Africa na anapata huduma nzuri ya kuutembelea. Mzungu akitoka ulaya hata marekani ticket ya ndege kwenda kenya ni rahisi sana kuliko ya tanzania, hoteli za kitalii kenya pia rahisi,pia kenya wana promotion tosha za utalii, sisi hoi kulalamika tu. Sisi watanzania tuko proud wenyewe wakati hatuna lolote, tumekalia tu rasilimali..sasa tuendeleeni tu tutafika.

    ReplyDelete
  7. TTB inatakiwa itoe video ya kukemea vikali kamili hiyo....Pia kama Tanzania tuna copyrights ya Owner....Je?kuna sheria ya ukiweza kushtaki nchi yeyote itakayohujumu?
    Kinachofanya mtu aogope kikuibia ni adhabu inayokuja kumtokea ......kama sivyo....ndio maana kila kukicha tunasikia Kilimanjaro iko Kenya....Diamond wa Kenya....
    Tunahitaji HATI MILIKI YA RESOURCES ZETU ZA TANZANIA

    ReplyDelete
  8. "Yawezekana katika mkutano huo wa vijana ambao mjumbe huyo wa nchi jirani alipata fursa ya kuzungumza na kufanya upotoshaji huo, wajumbe wa Tanzania pia walikuwepo ambao wangeweza kukosoa upotoshaji huo papo hapo na kuelezea ukweli na usahihi wa mahali ilipo Olduvai Gorge."

    Yawezekana? Why are u speculating? Umewasiliana na wajumbe hao? Someone at TTB was sleeping on the switch. This clip is a decade old! Suddenly, jerked from their slumber to a knee jerk reaction! Amazing?

    ReplyDelete
  9. Kaka mbona hatuambiwi huo mkutano ulikuwa wapi na nani walikuwa washiriki isije ikawa ni mtu katengeneza video nyumbani kwake nyuma ya bango la kimataifa kisha sisi sote tunampatia umaarufu.

    ReplyDelete
  10. Mwaka 2010 nikiwa Ukraine almanusura nimtoe ngeu jerani yangu na rafiki yangu aliyekua akijaribu kunishawishi mlima kilimanjaro wote ni wa nchi hiyohiyo ambayo mwandishi wa habari hii ameitambua kama nchi jerani, huyo jerani akanionesha mpaka jarida, sasa nipo mitaa ya scandinavian pia kuna mtu anatumia nguvu kutangaza serengeti ipo nchi hiyohiyo ya jerani........achilia mbali hiyo ukija ktk muziki na wanamuziki na hasa youtube ndio utachoka nyimbo nyingi zimezungushiwa mpaka bendera ya hiyo nchi jerani na kweli huku nje inaaminika kila kitu ni milki ya nchi hiyohiyo.......

    ReplyDelete
  11. Hawa jamaa TTB wanalalamika kwamba mjumbe wa Tanzania hakukanusha upotovu huo kwani wao sasa wamefanya nini? Si ndio yale majipu Magufuli alisema yameweka pesa nyingi kwenye akaunti zao kwenye Benki binafsi. Wazitumie kujitangaza na kukanusha wasisisngizie wengine.

    ReplyDelete
  12. Aliyesema uongo alikuwa anazungumza KIINGEREZA. kwanini wahusika wa TTB wanakanusha uongo huo kwa Kiswahili?

    ReplyDelete

  13. Ankal,

    Ni vizuri TTB wamejibu, ila hawajasaidia sana kwakuwa hata wao wamekosea. Olduvai iko Arusha, siyo Mkoa wa Manyara

    ReplyDelete
  14. TTB itumie mitandao ya Jamii Fb, twitter, YouTube na whatsapp kurekebisha kadhia hii duniani kote na sio kutupatia maelezo haya hapa. Pia, wawaandikie waandaji wa Mkutano ule sababu ule hautakuwa wa mwisho. Ili utakapokutana Mkutano mwingine au kny kaandaa repoti za mkutano ule masahihisho hayo yafanyuke. Vilevile, inasikitisha Kama kulikuwepo na washiriki kutoka Tanzania katika mkutano huo na wakaa kaa kimya mpaka kumaluzika kwa mkutano pasipo kurekebusha upotoshaji huo.

    ReplyDelete
  15. Ha ha ha! TTB kukanusha kwa Kiswahili madai yaliyotolewa kwa kizungu!!! Mbona unawapa mzigo wasiouweza! Ujanja wetu hapa hapa nyumbani! Yale Yale ya Maimuna😂😂😄 Wakishaandika kibongo ripoti nzito kwa Bodi kuhusu kazi kubwa waliyoifanya! Bongo tambarare sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...