NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa kwa Duka la dawa za binadamu la Shine Care Pharmacy lililopo Temeke, baada ya kubainika kuendeshwa kinyume cha sharia ikiwemo kutokuwa na kibali cha uendeshaji na mfamasia husika.

Dk. Kigwangalla ambaye aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Mfamasia Mkuu wa Serikali pamoja na msajili wa Baraza la famasia nchini na maafisa wengine, ambapo katika tukio hilo mapema leo Februari 29.2016, walikuta madawa mbalimbali yaliyokwisha muda wake na yale ambayo hayatakiwi kuuzwa katika duka kama hilo.

Aidha, Dk. Kigwangalla akitoa agizo la kufungwa kwa duka hilo, ameagiza kuchukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa Mahakamani mara moja il iwe fundishi na kwa maduka mengine yenye kufanya hivyo.

Kwa upande wake, Mfamasia wa Serikali, Bw. Henry Irunde amebainisha kuwa, dawa hiza za binadamu zilizokutwa hazifai kuuzwa katika maduka hayo na pia duka ambalo linaendeshwa bila kuwa na Mfamasia ni kinyume na sharia kwani watumiaji wakitumia dawa bila kuwa na maelezo ya kutosha kutoka kwa mtaalam wa dawa zinaweza kusababisha usugu kwa mwili wa binadamu n ahata kumsababishia matatizo.

Duka hilo la dawa ambalo lipo hatua chacche kutoka Hospitali ya Temeke, ni miongoni mwa maduka makubwa ya dawa za binadamu ambapo pia wachunguzi ha wa madawa ya binadamu walibaini kuwa milango mingi zaidi kinyume na ile inayotakiwa kuwa kwa maduka ya dawa hali ambayo walitilia mashaka huenda vitendo vingine vya kutoa huduma vinatumika licha ya kuwa milango hiyo ilifungwa kwa kile kilichoelezwa kuwa wahusika hawakuwapo.

Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, zoezi hilo la kukagua maduka ya dawa ni la nchi nzima na watazunguka nchi nzima kufanya ukaguzi huo bila kutoa taarifa hivyo kwa yeyote atakaekutwa anaendesha kinyume cha sharia atachukuliwa hatua stahiki.

Tazama  tv, Kuona video hiyo hapa: 
Imeandaliwa na Andrew Chale.
Naibu Waziri Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo ya kufungwa kwa duka hilo.
Baadhi ya maafisa walioambatana na Naibu Waziri wa Afya. Dk Kigwangalla wakimsikiliza kwa makini, Dk. Kigwangalla (hayupo pichani) wakati wa tukio hilo.
Mfamasia Mkuu wa Serikali Henri Irunde, akitoa taarifa yake ya ukaguzi katika duka hilo kwa wanahabari na Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla (Hayupo pichani).
(Picha zote na Andrew Chale.)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Siamini kama kukagua maduka ni kazi ya waziri. Kuna chombo husika hicho ndo akisimamie kitimize wajibu wake. Jaribu kutembelea hospitali za serikali ukiwa na fungu maalum la kutatua kero ndogo ndogo za dharura. Nakutakia utumishi mwema.

    ReplyDelete
  2. The mdudu, wewe mdau wa kwanza hapo juu tulia dawa ikuingiie itakua wewe ndio mwenye hilo#Duka so tulia watu wafanye yao ushauwa sana watanzania wezangu na midawa yako ya ajabu ajabu������������ unalo hilo hii serikali ya awamu ya 5 tia akili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...