JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA
RAIS IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemhamisha Bi.
Suzan Paul Mlawi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria,
kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Manejimenti ya utumishi wa umma
na Utawala Bora.
Taarifa
ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imeeleza kuwa uhamisho huo
umeanzia tarehe 26 Januari, 2016.
Taarifa
hiyo imeeleza kuwa pamoja na shughuli nyingine za Unaibu Katibu Mkuu, Bi. Suzan
Paul Mlawi, atashughulikia eneo la Utawala Bora.
Nafasi
ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria iliyoachwa wazi, haitajazwa
kwa sasa.
Gerson
Msigwa,
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar
es salaam.
01
Februari, 2016.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...