Efm 93.7 Radio kupitia kipindi chake cha Sports headquarters kimesheherekea kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake February 2015, hafla hiyo ilifanyika pale City Sports Lounge na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo akiwemo Waziri wa Habari, utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye kama mgeni rasmi. Nikipindi pekee kilicholeta mapinduzi zaidi ya michezo kwa utangazaji na uchambuzi yakinifu nchini.
Pichani Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye akikata keki ya birthday ya kipindi cha Makao Makuu ya
Michezo (Sports Head Quarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio jana
jijini Dar es Salaam.Kipindi hicho kimetimiza mwaka mmoja tokea kuanzishwa
kwake
Mkurugenzi Mtendaji wa EfmRadio Frances Ciza
akimlisha keki mgeni rasmi wakati wa hafla ya kutimiza mwaka mmoja kwa kipindi cha Makao Makuu
ya Michezo (Sports Head Quarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio
jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa na watendaji wa kipindi cha Makao Makuu ya
Michezo (Sports Headquarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio jana
jijini Dar es Salaam.Kipindi hicho kimetimiza mwaka mmoja tokea kuanzishwa
kwake
Watendaji wa kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Headquarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio wakiserebuka kwa furaha City Sports Lounge jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Simba SC Haji Manara akimsikiliza Afisa habari wa TFF,Baraka Kiziguto akihutubia kwenye hafla hiyo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...