Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Mamlaka hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza upande wa kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira akifuatiwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modest Kipilimba.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Mamlaka hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira akifuatiwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wizarani hapo, Haji Janabi. Wa tatu kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modest Kipilimba, anayefuata ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Avelin Momburi na Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho, Paul Bwathondi.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modest Kipilimba akijitambulisha kabla ya kuanza kikao cha Watendaji Wakuu wa NIDA pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kikao hicho kilichoitishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na anayefuata ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Kitwanga katika watu hawana uzalendo ni hao watu wa NIDA kiukweli wanatusumbua saaana unaenda leo kuzaja form zao kunaondoka wanakuambia urudi siku Fulani siku ukirudi unaambia bado tunahitaji taarifa zako Fulani hivi hawana misingi ya kazi hiyo ya vitambulisho vya Taifa mbona tulivyokuwa tukiomba passport pale Uhamiaji ukifika unaambiwa zinatakiwa taarifa Fulani na Fulani ukikamilisha taratibu zinafanyika na wanakuambia baada ya mda Fulani passport yako inakuwa tayari. Binafsi nakuomba na kukushauri waeleze watendaji wakuu wa NIDA watutangazie taarifa zipi zinahitajika wanachotakiwa kufahamu kuna watu wanaishi Dar Es Salaam lakini wanafanyia kazi mikoani kuna kipindi wanakuambia njoo siku flani we upo mkoani kiukweli wanasumbua na inaonesha kabisa hakuna msingi na taratibu uliowekwa ili Mtanzania apate Kitambulisho cha Taifa. Naomba uwekwe utaratibu kuwa ili upate kitambulisho hiki cha Taifa tunaomba uwe na taarifa kadhaaa sasa muhusika akifika pale wao NIDA kama wataalamu watamchukua na maelezo mengine kuhakikisha kuwa muombaji ni Mtanzania halisi kasha taratibu zinafanyika za muhusika kupata kitambulisho chake lakini mtu unafatilia kitambulisho kama unafatilia kazi jamani tubadilike tuipeleke Tanzania yetu mbele tufanye kazi kwa misingi na taratibu ili tusiwe tunapoteza muda kwa kitu kimoja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...