Afisa
Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa 3 kushoto) akimkabidhi
Kanizio Annatory (katikati) ambaye ni miongoni mwa vijana waliowezeshwa
na mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” mashine na vifaa vya kuoshea
magari pamoja na sehemu ya kisasa ya kufanyia biashara, akishuhudiwa na
ndugu zake pamoja na wafanyakazi wa Airtel katika hafla iliyofanyika
kijiji cha Kamnazi mkoani Kagera.
Afisa
Uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kwanza kulia) pamoja na
wafanyakazi wa Airtel wakimwonesha Kanizio Annatory (wa pili kushoto)
sehemu ya kisasa ya kuosha magari aliyowezeshwa na mpango wa Airtel
Fursa “Tunakuwezesha” baada ya kukabidhiwa mashine na vifaa vya kuosha
magari katika hafla iliyofanyika kijiji cha Kamnazi mkoani Kagera.
Mwanzoni
mwa wiki hii Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa iliweza
kufika katika kijiji cha Kumnazi wilayani Ngara mkoani Kagera na
kumfikia Kijana Kanizio Annatory anayejishughulisha na biashara ya
kuosha magari, kwa kumpatia vifaa na kufanyiwa ukarabati wa eneo lake la
kazi . Vijana wengi wanaamini maisha mazuri na fursa za kiuchumi
zinapatikana mjini, lakini kwa Kijana Kanizio kupita kwa barabara katika
kijiji hiki ni fursa adhimu kwake.
Airtel
Fursa umelenga katika kuwezesha vijana wajasiriamali hapa nchini kwa
kutoa msaada kwa vijana ambao wanaonyesha juhudi ya kujikomboa na
changamoto za maisha katika Jamii zinazowazunguka kwa kuwapatia vitendea
kazi na kutoa mafunzo ya biashara ya ujasiriamali. Airtel Fursa ni moja
ya sehemu ya utekelezaji wa wajibu wa Airtel katika kurudisha sehemu
ya faida wanayoipata kwa jamii ili kukidhi matakwa ya kiuchumi, na
kuunga mkono jitihada za serikali katika kubadilisha maisha ya wananchi.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...