Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) nchini Kenya, Mhe. TADUMI ON'OKOKO, kwenye Ubalozi wa DRC Nairobi leo, Mhe. ON'OKOKO, ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao Kenya, alifariki dunia tarehe 20 Machi 2016 huko Paris, Ufaransa, ambako alikuwa anatibiwa. Anayeshuhudia ni Kaimu Balozi wa DRC, Mhe. Michel Mubare, ambaye alifahamisha kuwa marehemu atazikwa Kinshasa baada ya mipango kukamilika.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule (Kulia) akimfariji Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mhe. Michel Mubare, baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Balozi wa nchi hiyo Kenya, Mhe. Tadumi On'okoko jijini Nairobi leo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...