Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya Afisa mtendaji mkuu wa Benki ya Barclays Afrika , Maria Ramos na waandishi hao kwa njia ya simu ya mezani akiwaAfrika Kusini kuhusiana na benki hiyo kuongeza wateja wake wa bara la Afrika hasa katika nchi za Afrika Kusini, Botswana, Ghana na Zambia ikiwa benki hiyo inawateza zaidi ya 885,000 kwa bara la Afrika na kuongeza mapato yake kwa asilimia 10, Ikiwa kwa bara la Afrika  Maria amesema kuwa inakabiliwa na changamoto nyingi katika ufanyaji wa biashara hasa katika kutokupata wafanyakazi wachapakazi, umasikini na kutokua na usawa katika ufanyaji wa  biashara ya benki.
Kutoka kulia ni Afisa Masoko wa benki ya Barclays Tanzania, Joe Bendela akisikiliza kwa ukaribu katika simu ya mezani ambayo ilitumika kuongea na Afisa mtendaji mkuu wa Benki ya Barclays Afrika, Maria Ramos akiwa afrika Kusini leo wakati wakiongea na waandishi wa habari wa jijini Dar es Salaam. Aidha Maria amesema kuwa Benki hiyo barani Afrika imeongeza mapato yake kwa asilimia 10 .
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...