Klabu maarufu ya kuogelea jijini, Dar Swim Club imewapongeza waogeleaji wake kwa kufanya vyema katika mashindano ya taifa ya kuogelea yaliyomalizika hivi karibuni katika bwawa la Hopac.

Akizungumza jijini jana, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Inviolata Itatiro alisema kuwa waogeaji wake wameweza kuboresha muda wa kuogelea na kuiwezesha klabu hiyo kutwaa nafasi ya kwanza kwa upande wa wanawake kwa kukusanya jumla ya pointi 1,964.50.

Inviolata alisema kuwa kwa upande wa wanaume, walikusanya jumla ya pointi 1,086.50 na kushika nafasi ya pili. Alisema kuwa wamefarijika na matokeo hayo kutokana na wao kuwakilishwa na waogeleaji chipukizi katika mashindano hayo.

“Hii ni faraja kwetu, tumeweka mikakati ya kukuza mchezo wa kuogelea kwa miaka 10, tunawaogeaji wadogo sana lakini wana vipaji vya hali ya juu, lakini kutokana na mfunzo mazuri ya makocha wetu, wameweza kuwashinda waogeleaji wenye umri mkubwa, kwa kweli wanastahili pongezi,”.

“Wakati tunaanza, hatukutegemea kufikia hatua hii, tuliweza kutwaa medali 94 katika mashindano ya kuogelea ya Taliss na kushika nafasi ya kwanza na kuwa klabu bora, natoa wito kwa wazazi ambao wanataka watoto wao kujua kuogelea na kushindana katika mashindano ya ndani na kimataifa, kujiunga na klabu yetu,” alisema Inviolata.
Alisema kuwa mafanikio ya klabu yao yametokana na ushirikiano wao na wazazi na wadhamini mbalimbali ambao wamekuwa nguzo kubwa ya kufanikisha mambo kadhaa ya maendeleo ya mchezo wa kuogelea.

“Tuliweza kufanya semina kwa makocha na waogeleaji wetu chini ya mkufunzi wa kimataifa na muogeleaji nyota wa zamani wa Olimpiki, Penny Heyns wa Afrika Kusini. “Mafunzo yalikuwa ya kisasa na sasa tunajivunia matunda yake, nawashukuru makocha kwa kufanya kazi kubwa,” alisema.

Alisema kuwa makocha wao, Michael Livingstone, Ferick Kalengela, Radhia Gereza, Kanisi Mabena, Adam Kitururu, Simon Ngoya na Salum Mapunda wamekuwa nguzo kubwa ya kufikia malengo yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...