Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco) limebaini wizi mkubwa wa Maji kwenye eneo la
Oysterbey mtaa wa Msasani Rd wakati wa operesheni maalumu yakubaini wezi wa Maji kwenye majengo
makubwa Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye tukio hilo, Meneja wa Dawasco Kinondoni Bi Judith Singinika alieleza kuwa kwenye
operesheni hiyo maalum inayoendelea kutokana na Agizo la Mh. Waziri wa Maji kukagua Majengo yote
Makubwa pamoja na viwanda Jijini Dar es Salaam ilikubaini vyanzo vyake vya Maji ,ndipo walipobaini wizi
mkubwa wa Maji mtaa wa Msasani Rd kwenye jengo hilo la ghorofa lenye nyumba ndogo(apartments) 25
linalomilikiwa na Chuo cha Biashara (CBE) ambapo kulikutwa na laini mbili zinazoleta Maji na laini moja
ikiwa haina mita na ndiyo ilikuwa inafanyiwa Matumizi makubwa.
Pia meneja huyo wa Dawasco ameeleza kuwa wamechukua hatua za kisheria kwa kukitoza chuo hicho
faini ya Shilingi milioni 100 ambapo inatakiwakulipwa ndani ya miezi 24 hivyo kila mwezi wanatakiwa kulipa
kiasi kisichopungua shilingi milioni 4160000.
“Katika operesheni yetu maalum ya kubaini wezi wa Maji tumeweza kubaini wizi mkubwa wa Maji
Oysterbay Kwenye jengo linalomilikiwa na chuo cha biashara (CBE) ambapo wakufuzi wa chuo hicho ndio
wanaoishi humo na tumekuta kuna laini mbili zinazoleta Maji moja ina mita na nyingine haina na ndio ina
matumizi makubwa hivyo tumewatoza faini na wakubali kuilipa ndani kwa awamu ndani ya miezi 24”,
alisema Singinika.
Hata hivyo Dawasco inaendelea kuwasihi wamiliki wote wa Majengo makubwa ya ghorofa pamoja na
viwanda waliojiunganishia huduma ya Maji kiholela kijisalimisha kwani operesheni hiyo ni endelevu na hatu
kali za kisheria zitachukuliwa kwa yoyote atakaye kamatwa.
Bomba la Maji lilounganishiwa kiholela ambalo halina mita linalopeleka huduma ya Maji kwenye jengo kubwa la ghorofa ambalo linamilikiwa na Chuo cha Biashara (CBE) eneo la Oysterbay mtaa wa Msasani Rd Jijini Dar es Salaam.
Maofisa wa Dawasco Kinondoni waking’oa laini ya Bomba la Maji lilounganishiwa kiholela lisilo na Mita kwenye jengo kubwa la ghorofa linalomilikiwa na Chuo cha Biashara (CBE) eneo la Oysterbay mtaa wa Msasani Rd Jijini Dar es Salaam.




Masaki vipi? Slipway?
ReplyDeleteJe wafanyakazi wa DAWASCO wanapoomba hongo ili wasikushitaki niaje?
ReplyDelete