Na  Bashir  Yakub.
Mara  kadhaa  tumeeleza  mambo  mbalimbali  ya kisheria kuhusu  mikopo , waomba mikopo  na  watoa  mikopo.  Haki  na  wajibu  ni  vitu  ambavyo  mara  nyingi  vimeguswa. Hii  ni  kwasababu  eneo  hili  ni  katika  maeneo  tata. 

Ni tata kwa  pande  zote  yaani taasisi  za  fedha halikadhalika  wachukua  mikopo.  Iko  sintofahamu  nyingi  hasa  kwa  wachukua  mikopo. Mara  nyingi  hawa  hujikuta  katika  matatizo   na  wakati  huo  eti  ndio  hufahamu  haki   na  wajibu  wao.
Baada  ya  tatizo  kutokea  ndipo  hujua  walitakiwa  kufanya nini  huko  nyuma. Bahati  mbaya muda  huo huwa  wamechelewa  tayari. 

1.SUALA  NA  KUWA  NA  MKE/MME WAKATI  WA  KUCHUKUA  MKOPO.
Wakati  wa  kuchukua  mkopo  ni  wakati  ambao  taasisi  inayotoa  mkopo  humtahini ( interview)  mchukua  mkopo. Kila  taasisi  yaweza  kuwa  na  maswali  ambayo  yana tofauti  na  taasisi  nyingine. Maswali hutokana na   na taarifa ambazo  taasisi ingependa  kujua  kutoka  kwa  mchukua  mkopo. 

Hata  hivyo  pamoja  na  utofauti  huo bado   yapo  maswali  ya  msingi ambayo  kila  taasisi  utakayoenda  kuchukua  mkopo  ni  lazima  utaulizwa.  Haya  ni  yale  yatokanayo  na  sheria zinazohusu  masuala  ya  mikopo.  Ni maswali  yanayofanana( common  questions).

Moja  ya  maswali  haya  ni  swali  hili   la  kutaka  kujua  kama  muomba  mkopo  ana  mwenza kwa  maana  ya  mke  au  mme.  Hili  ni  swali  la  kisheria  ambalo   lina  athari  na  matokeo  ya  kisheria  kama  tutakavyoona  hapa . 

2.UPI  UMUHIMU  WA  KUJUA IWAPO MWOMBA  MKOPO  ANA  MME/MKE.

Hii  ni  kwasababu  unapochukua  mkopo   mara  nyingi  hutakiwa  kuweka  rehani.  Na  rehani  inayokubalika  huwa  ni  mali  isiyohamishika  ambayo  ni  nyumba au  kiwanja. Na  mara  nyingi nyumba  au  kiwanja  ni  mali  ambazo  huhesabika  zinamilikiwa  kwa pamoja kati ya  mme  na  mke  ikiwa  wameoana. 

Kwa  maana  si  ruhusa  kwa  mmoja  wa wanandoa  hao  kuweka  rehani  mali  hizo  bila  mwingine kuridhia. Na  ikitokea  kuwa mmoja  hakuridhia  basi  hupata  haki  ya kusitisha  mali  hiyo  kuhusishwa  katika  mkopo.

Hatua  hiyo  inaweza  kuwa  hasara  kwa  mtoa  mkopo. Basi  kutokana  na  hilo huibuka  umuhimu mkubwa  wa  kujua  iwapo  mwomba  mkopo   ana  mke/mme.

KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...