Waungwana kila uchwao kwenye jiji hili na viunga vyake sambamba na maeneo mengi ya nchi, kuna neno wa ‘kimataifa’ hulisikia likiimbwa.

Waimbaji wakuu wa neno hilo ni mashabiki wa Yanga wakiongozwa na mpiga zumari wao aliyeacha kazi yake na kujigeuza muimbaji.

Kinyume chake hilo neno klabu ya Simba huitwa wa ‘mchangani’ au wa ‘matopeni’. Wengi wananilaumu kuwa kwa nini huwa sijibu neno lolote la ajabu kwa Yanga. Jibu langu ni jepesi tu, lazima tujitofautishe msemaji wa klabu na mropokaji wa klabu.

Mimi hupenda kuzungumzia issues sio porojo au lugha za uchochoroni. Haiwezekani nikawa kiongozi kisha nikaongea lugha za mashabiki ‘maandazi’.

Kwa hiyo mtaniwia radhi wapenzi wa mpira kwa kutokuwa muimbaji wa ngonjera za uchochoroni. Mara zote nitabaki msemaji wa klabu kubwa nchini na ntaongea facts kwa kadri zilivyo.

Wadau zisomeni sifa za kimataifa kwa klabu ya Simba nje ya nchi halafu zifananisheni na timu nyingine nchini.

Walau kama zitafikia nusu tunawaruhusu watafute tusi jipya. Ombi langu kwenu isambazeni taarifa hii katak kila mtandao wa kijamii kisha waseme wao wanaojiita wa kimataifa.

Simba ndiyo timu ya kwanza nchini kupanda ndege na hii ilikuwa mwaka 1963 tena wakati huo taifa la Tanzania halikuwa limeundwa, ilikwenda Ethiopia kwa mwaliko wa rais wa taifa hilo Haile Selassie
Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa jezi na hii ilikuwa 1938 ilipocheza na kombaini ya mabaharia wa meli zilizotia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam.

Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa viatu nchini na hii ilikuwa1949 ilipocheza na kombaini ya jeshi la majini Navy ya Afrika Kusini.
Simba ndiyo timu ya kwanza kuwa na basi lake yenyewe na hili lilinuliwa mwaka1968.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Timu ya kimataifa ni ile i ayoshiriki mashindano ya kinataifa ambao kwa sasa ni yanga na azam kwa hiyo acha porojo za mabasi ya nwaja 68 ukiwa hujazaliwa

    ReplyDelete
  2. Huyu bwana nawafananisha na waleee wazee wetu wa zamaaani waliokua na gari kama vile mgongo wa chura , combi zilipoharibika waliamua kuziweka uwani mpaka leo ili kulinda heshima......hahahaha kwa sasa zinahesabika ni uchafu tu. Acha kulia lia wewe wa kitopeni tu a.k.a mchangani na mtasubiri sana ................

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...