Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba akisalimiana na na kuwashukuru Wananchi wa Kijiji cha Mpunda pamoja na kijiji cha Kihitu vilivyopo Kata ya Vuga kwa kumchagua kuwa Mbunge wao kwa mara nyingine tena na pia kwa kumchagua Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa awamu ya tano kupitia chama cha Mapinduzi (CCM).
Mh Makamba pia alifanya ziara a ya kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo sambamba na kupokea kero za Wananchi hao na kuzitafutia ufumbuzi,pia amewahidi wananchi hao kuwaletea zaidi Maendeleo katika jimbo hilo.(Picha na Imani Nsamila) .


Wananchi
wa Kijiji cha Mpunda Kata ya Usambara wakimuonesha Mbunge wa Jimbo la
Bumbuli January Makamba eneo ambalo Wakazi hao wamepewa na Kiwanda cha
Katani ili wajenge Zahanati ya Kijiji.

Katibu wa Wilaya ya Lushoto Ramadhani Mahanyo akizungumza katika Mkutano huo.

Mbunge
wa Jimbo la Bumbuli January Makamba akisalimiana na Wananchi wa Kijiji
cha Mpunda baada ya kumalizika kwa Mkutano huo,ambapo pia aliwashukuru
Wananchi hao kwa kumchagua kuwa Mbunge wao kwa kura nyingi,ane amewahidi
kuwaletea maendeleo katika jimbo hilo la Bumbuli.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...