Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka
kulia) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa mgodi. Wa kwanza kulia ni
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Zelothe Stephen
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto)
akiwasili katika mgodi wa dhahabu wa Cata Mining. Kulia ni Mkurugenzi wa
mgodi huo, Mahuza Nyakirang’ani.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati)
akikagua shughuli zinazoendelea mgodini hapo. Kushoto kwake ni Meneja wa
mgodi huo, Peter Bourhill na kulia kwake ni Mkurugenzi wa mgodi,
Mahuza Nyakirang’ani.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
akisalimiana na baadhi ya wananchi kutoka vijiji vya jirani na mgodi wa
Cata Mining waliohudhuria mkutano wake wa hadhara ili kujadili masuala
mbalimbali.
Meneja wa mgodi wa Cata Mining, Peter Bourhill akimweleza jambo Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipokua akikagua mgodi
huo. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa mgodi, Mahuza Nyakirang’ani.
Prof. Muhongo aagiza Malipo ya Ushuru wa Huduma yafanyike hadharani
Serikali imeagiza ulipaji wa ushuru wa huduma unayofanywa
na migodi mbalimbali nchini ufanyike hadharani ili kila mwananchi aelewe
kiasi kilicholipwa.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
alitoa agizo hilo hivi karibuni alipofanya ziara kwenye mgodi wa dhahabu
wa Cata Mining uliopo katika kijiji cha Kataryo, mkoani Mara ambapo
vilevile alikagua shughuli za mgodi huo na kuweka jiwe la msingi.Profesa Muhongo alisema ili kuondoa hali ya sintofahamu
pamoja na kuongeza uwazi na utekelezaji sahihi wa miradi kutokana na
fedha zitokanazo na malipo ya ushuru wa huduma, ni lazima ulipaji huo wa
ushuru husika ukashuhudiwa na kila mwananchi.
Aliongeza kwamba wananchi wanapaswa kushirikishwa katika
kuibua miradi itakayotekelezwa kwa kutumia fedha hizo za ushuru wa
huduma.“Wananchi wanapaswa kuelewa ni kiasi gani kimelipwa; na hiyo haitoshi inatakiwa washirikishwe kwenye matumizi ya fedha hiyo.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...