NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
SHIRIKA la ugavi wa umeme Tanesco Mkoani Pwani limewakamata watu
saba kwa tuhuma za wizi wa umeme katika
eneo la kwamfipa Wilayani Kibaha ambao
walikuwa wamehujumu miundombinu kwa kujiunganishia umeme kinyemela kinyume cha
utaratibu.
Akizungumzia kuhusina na
tukio hilo Afisa Usalama wa Tanesco Mkoa wa Pwani Herny Byarugaba
amesema
kwamba kubainika kwa watu hao waliokuwa wanaiba umeme kumetokana baada
ya kupatiwa taarifa kutoka kwa wananchi wasamalia wema wa eneo hilo.
Byarugaba amesema kwamba
wezi hao walikuwa wamezichimbia
nyaya za umeme chini ya barabara ya kuusambaza katika baadhi ya maeneo ikiwemo
maduka, mabanda ya kuonenyeshea video hali ambao amedai ni hatari kwa usalama
wa maisha ya watu kwani kunaweza kutokea majanga ya kuungua kwa nyuma za watu
na kupoteza maisha yao.
“Sisi tumepata taarifa hizi kutoka kwa wananchi wasamalia
wema kwa hiyo sisi kama tanesco tukaamua kufanya msako mkali katika eneo hili
la kwa mfipa na kuweza kukuta wateja wetu wameamua kutumia njia za kinyemela
kwa kuiba umeme na mbaya zaidi nyaya wamezipitishia chini kabisa ya barabara
hivyo hali hii ni hatari sana watu wanaweza kupoteza maisha,”alisem Byarugaba.
Aidha alibainisha kwamba kutokana na kujiunganishia umeme
kinyume na taratibu kunaweza kuleta madhara makubwa kwa wananchi kwani pindi mvua inaponyesha na nyaya hizo
zikiwa zimechunika maji yanashika umeme na hivyo kunaweza kusababisha hatari kubwa sana.
Pia Byarugaba aliongeza kuwa Shirika la Tanesco limekuwa linapata hasara kubwa na
kupoteza mapato yake kutokana na baadhi ya watu kuamua kufanya vitendo vya hatari vya kuhujumu
miundombinu yao pamoja na kuiba umeme.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa serikali ya mtaa kwamfipa Juma Tanga ambaye alifika eneo la tukio alisema
kwamba amesikitishwa sana kuona baadhi ya wananchi wake kushiriki kuiba umeme
kinyume na taratibu na kuwataka waachane na vitendo hivyo kwani ni hatari kwa
usalama wa maisha yao.
Mwenyekiti huyo alisema kwamba katika kukabiliana na hali hiyo atahakikisha
anaweka mikakati ya kuwaelimisha wananchi wake katika mikutano mbali mbali
kuhusina na madhara ambayo yanaweza
kujitokeza kutokana na kujiunganishai umeme bila ya kuzingatia taratibu
zilizowekwa na wahusika wenyewe.
Naye Meneje wa
Tanesco Mkoa wa Pwani Martin Madulu ametoa tahadhari kwa wananchi
wote wa Mkoa wa Pwani kuachana kabisa na tabia
ya kujiunganishia umeme pasipo kuwatumia wafanyakazi husika wa tanesco
na
badala wake wahakikishe wazingatie
taratibu katika kuunganishiwa umeme katika sehemu za biashara pamoja na
nyuma
za kuishi.
Aidha katika hatua nyingine Mejeja huyo aliwataka wananchi
kujihadhari ya matapeli ambao wanajifanya ni wafanyakazi wa shirika hilo na
endapo wakiwabaini watoe taarifa mapema katika vyombo vinavyohusika ili sheria
iweze kufuata mkondo wake.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika hilo wakiwa
katika eneo hilo mara baada ya kubaini kuwepo kwa wizi huo wa umeme(PICHA NA
VICTOR MASANGU).
Afisa Usalama wa shirika la ugavi wa umeme
Tanesco Mkoa wa Pwani Henry Byarugaba akionyesha moja ya eneo ambalo wameiba
umeme kwa kujiunganishia bila ya
kuzingatia taratibu.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...