Hatua nyingine kubwa
imefikiwa leo hii katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha
mafuta ghafi kutoka Uganda kupitia Kaskazini mwa Tanzania hadi bandari ya
Tanga.
Katika kikao kazi kilichofanyika jijini Arusha, Waziri wa Nishati na
Madini, Prof. Sospeter Muhongo, Waziri wa Maendeleo ya Nishati na
Madini-Uganda, Mhandisi Irene Muloni, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James
Mataragio na Meneja Mkuu wa Total E&P Uganda, Ndugu Adewale Fayemi wametia
saini mpango wa pamoja wa utekelezaji wa mradi huo (Project Implementation Plan).
Hatua hii imekuja ikiwa ni wiki mbili
tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais
wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kutoa tamko la pamoja la utekelezaji wa
mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda kupitia
mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma hadi bandari ya
Tanga.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio (wa kwanza kushoto), Waziri wa Nishati
na Madini-Tanzania, Prof. Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kushoto), Waziri wa
Maendeleo ya Nishati na Madini-Uganda, Mhandisi Irene Muloni ( wa tatu kutoka
kushoto), Meneja Mkuu wa Total E&P Uganda, Adewale Fayemi (wa nne kutoka
kushoto) wakitia saini mpango wa pamoja wa utekelezaji wa mradi wa bomba la
kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga. Kulia kabisa ni
Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Nishati na Madini-Uganda, Dkt. Kabagambe
Kaliisa
Waziri
wa Nishati na Madini-Tanzania, Prof. Sospeter Muhongo na Waziri wa Maendeleo ya
Nishati na Madini-Uganda, Mhandisi Irene Muloni wakibadilishana nyaraka baada
ya kutia saini kwa pamoja
Waziri
wa Nishati na Madini-Tanzania, Prof. Sospeter Muhongo na Waziri wa Maendeleo ya
Nishati na Madini-Uganda, Mhandisi Irene Muloni wakionesha nyaraka zenye mpango
kazi wa pamoja kati ya Tanzania, Uganda na Kampuni ya Total na TPDC juu ya
utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka
Uganda hadi bandari ya Tanga.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...