Na Mwandishi Maalum, New York
Wajumbe wa Mkutano wa 60 wa Kamisheni kuhusu hali ya wanawake, wanaendelea na majadilino juu ya dhima ya
uwezeshwaji wa wanawake na uhusiano wake katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ( Agenda 2030).
Akichangia majadiliano hayo,Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe. Ummy Mwalimu ( Mb) anasema
Tanzania inatambua kwamba uwezeshwaji
wa mwanamke na mtoto wa kike ni muhimu sana katika kufanikisha utekelezaji
wa Agenda 2030.
Na kwamba ili kufanikisha
hilo, Serikali inaendelea na jukumu la
kuhusisha na kuingiza Ajenda
2030 katika mifumo
iliyopo ya kisera, mipango na
mikakati ya kitaifa ya maendeleo.
Waziri Ummy Mwalimu
anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu, amebainisha pia kwamba
Serikali inapitia kwa makini
lengo namba tano la agenda 2030 ambalo linazungumzia umuhimu wa
kufanikisha usawa wa kijinsi na uwezeshaji wa wanawake wote na wasichana.
Akaeleza zaidi kwamba
uamuzi wa serikali kufanya marejeo ya mikakati Na mipango ya kitaifa inalenga kuhakikisha kwamba usawa wa
jinsia na uwezeshwaji wa wanawake
unaendelea kuwa kipaumbele cha nchi.
Vilevile amesema,
ushiriki jumuishi umefanyika
katika kubuni viashiria ambavyo
vinaendana na mahitaji ya nchi na vinaweza kutumika mpaka ngani za chini katika upimaji wa utekelezaji wa Agenda 2030.
Katika kuelezea zaidi uzoefu wa Tanzania katika uwezeshwaji
wa mwanamke na msichana wa kitanzania.
Waziri pia alianisha sheria
mbalimbali zinazolimda mwanamke na mtoto wa kike dhidi ya ukatili au ubaguzi wa aina yoyote ile , kuanzishwa kwa mifuko na Banki za kuwawezesha
wanawake kujipatia mikopo kwa riba nafuu, uboreshwaji wa huduma za afya
hususani afya ya mama na mtoto pamoja
na fursa sawa za ajira zenye staha na
fursa za kujiajiri.
Pamoja na
kueleza namna Serikali inavyoendelea kujipanga katika
utekelezaji wa Agenda 2030, Waziri Mwalimu amesema ili utekelezaji huo uwe na mafanikio
tarajiwa, ushirikiano na
wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja
sekta binafsi utahitajika sana.
Na
akatumia nafasi hiyo kuwashukuru wadau
hao ambao wamekuwa wakishirikiana na
Serikali katika maeneo
mbalimbali
Baadhi ya changamoto ambazo amesema Tanzania inakumbana
nazo katika jukumu hilo la uwezeshwaji
wa wanawake na wasichana pamoja na vikwazo vya kimila na kitamadani
anavyokumbana navyo mwanamke na mtazamo
hasi dhidi ya wanawake.
Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb.)wakati akitoa taarifa ya nchi katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake Duniani (CSW).
Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb.) akiwa Ubalozini New York na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Peter Serukamba (kushoto na Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Tuvako Manongi baada ya kuwasilisha taarifa ya nchi katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake Duniani (CSW).





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...