Uzinduzi
wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika
la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Dodoma siku ya Jumanne
na Jumatano, Machi 22-23, 2016.
Mradi
huo ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening (PS3) ni
wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 97
katika mikoa 13 ya Tanzania bara.
PS3
inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha
mifumo ya sekta za
umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa
taarifa, na tafiti tendaji. Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya
Serikali kuu na Halmashauri, una nia ya
kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo
hazijanufaika vya kutosha.
RC wa Dodoma, Jordan Rugimbana, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3
Katika
uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana,
na uzinduzi
ulihudhuriwa pia na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Dodoma ambaye amehamishiwa mkoa wa
Songwe, Chiku Galawa. Watu takribani 180
walihudhuria. Washiriki wa uzinduzi huo walikuwa
ni: Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Wakuu wa Wilaya za Dodoma, Wenyeviti wa Halmashauri,
Wakurugenzi wa Halmashauri, Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa, na Wajumbe wa Timu ya Mejenimenti kutoka kwenye
Halmashauri.
Mkoa
wa Dodoma una Halmashauri nane, ambazo
ni Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Halmashauri
ya Wilaya ya Bahi, Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa,
Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, na Halmashauri
ya Mji wa Kondoa.
PS3
ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na
Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID.
Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo
ni: Abt Associates Inc., kama
mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ambao ni Taasisi ya Benjamin Mkapa
(BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzi ya Serikali za
Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute,
Intra Health International, na Urban Institute.
Mikoa
13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni: Iringa, Dodoma, Kagera,
Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na
Shinyanga.
Mkurugenzi wa Mradi wa PS3, Dk. Emmanuel Malangalila, akitoa mada kwenye uzunduzi wa mradi wa PS3 mkoani Dodoma
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...