MBUNGE wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Vicky Kamata (Viti maalum CCM) amesema kwamba amejisikia furaha na ana kila sababu ya kuiomba kampuni ya
Msama Promorions kutimiza ahadi yake ya kulipeleka Tamasha la Pasaka mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Alisema
kuwa mbali na burudani naamini kuwa hata wananchi watanufaika na Tamasha hilo
kwa ujumbe kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kuhusiana na mauaji ya walemavu wa ngozi 'albino' pamoja na vikongwe.
Kwa
kweli mauaji hayo yanatokana na imani ya kishirikina lakini kwa tamasha hili
ambalo ni sawa na kutangaza injili kwa njia ya nyimbo itaweza kuvunja nguvu za
kishetani na wananchi kumrudia mungu.
“Nimefurahishwa
katika hili naamini nguvu ya mungu itaenda kutenda kazi yake hivyo ni imani
yangu kuwa watu watabarikiwa kwa kuvunja nguvu ya shetani na watu kumrudia
mungu ,” alisema Mbunge huyo ambaye pia ni msanii.
Aidha
Mbunge huyo alisema angefurahi kama waimbaji ambao wametajwa katika
tamasha hilo kama Rose Muhando, Bonny Mwaitege na Upendo Nkone wafike Geita na
wamewaandalia mapokezi ya aina yake kwani wana idadi kubwa ya mashabiki.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...