Wafanyabiashaa wadogo wa jijini Mwanza, wameishukuru Benki ya CRDB, kwa kupitia Kampuni yake Tanzu ya CRDB Microfinance Limited, imewawezesha wafanyabiashara kupatiwa mikopo ya riba nafuu na bila dhamana kitendo ambacho wamekiita ni ukombozi mkubwa kwa wafanyabiashara wadogo, hivyo kuuita benki ya CRDB ni Benki Mkombozi.
Rai hiyo imetolewa na wafanyabiashara wa soko la samaki la Mwaloni,Kirumba, walipotembelewa na Maofisa wa Benki ya CRDB, kufuatilia maendeleo yao ya kibiashara na kusikiliza shida zao na kujua mahitaji yao, katika kuelekea kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya benki ya CRDB yatakayofikia kilele mwezi Juni mwaka huu.
Wakitoa ushuhuda wao mbele ya mwandishi wa habari hizi, wafanyabiashara hao wanaofanya biashara zao kwenye soko la samaki la Mwaloni Mwanza, wamesema mikopo ya CRDB yenye masharti nafuu na riba ndogo, imewawezesha kunyanyuka kibiashara kutoka kuwa wafanyabiashara wadogo, kuelekea kuwa wafanyabiashara wa kati.
Akizungumza kwa niaba ya wenzeke, mmoja wa wafanya biashara hao Dionizi Muganyizi Kato, ameishukuru CRDB Bank na kutoa ushuhuda kuwa yeye alianza na mkopo wa Sh 300,000 kutoka benki hiyo ukiwa ni mkopo wa vikundi, amekuwa akiendelea kukjopa na kulipa hadi akahitimu na kutoka kwenye kikundi na kuanza kuchukumkua mkopo binafsi ambapo sasa anatarajia kuchukua mkopo wa Sh Milioni 7 ili aweze kujiimarisha zaidi kiuchumi.
“Nawashukuru sana Benki ya CRDB, kupitia huduma zao za mkopo wameniwezesha nimeweza kujenga nyumba ya kisasa ya vyumba sita, nimesomesha kijana wangu hadi Chuo Kikuu ila ombi langu kwao waniwezeshe mkopo wa gari aina ya Pick up ili niondokane na changamoto ya usafirishaji”, alisema Bw. Kato.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa CRDB mkoani Mwanza Hamis Swalehe alisema kuwa benki inafanya kazi karibu na wafanyabiasha ndogo ndogo, na imeanzisha programu maalum ya kuwawezesha wateja wadogo wanaopata huduma za kifedha kutoka CRDB ili wawe wateja wakubwa.
“ Sisi CRDB tunawawezesha wafanyabiashaa wadogo wakue kwa kutumia huduma zetu za kibenki na kupitia mpango huo tumewezesha zaidi ya wafanyabiashara wadogo wadogo 2000 jijini Mwanza kupitia vikundi na mtu mmoja mmoja, ambapo kila mwanakikundi anakopeshwa kuanzia Sh 200,000 na Benki hiyo imetoa mikopo ya thamani ya Sh Bilioni 1 kwa wafanyabiashara hao wadogo wadogo”, alisema na kuongeza kuwa kupitia uwezesho huo wajasiriamali wengi wana uelewa mkubwa wa mambo ya fedha na mikopo.
Mmoja wa wafanyabiashara ya samaki, wa soko la Mwaloni, Kirumba, Mwanza, Dionizi Muganyizi Kato, akionyesha moja ya bidhaa zake za samaki, ameishukuru CRDB Bank kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu na riba ndogo, imewawezesha kunyanyuka kibiashara kutoka kuwa wafanyabiashara wadogo, kuelekea kuwa wafanyabiashara wa kati.
Mmoja wa wafanyabiashara ya mkaa, wa soko la Mwaloni, Kirumba, Mwanza, Gati Mwita, akizungumza na Mwakilishi wa gazeti la Daily News, Kanda ya Ziwa, Mwanza, Pius Rugonzibwa, kuhusu jijnsi benki ya CRDB ilivyompatia mkopo wa kikundi wenye masharti nafuu na riba ndogo,umewawezesha kunyanyuka kibiashara kwa kumuongezea mtaji hivyo kuweza kuhudumia wateja wengi zaidi na kuongeza kipato chake na kukuza biashara yake.
Mwakilishi kutoka ubalozi wa Kanada nchini Tanzania, Ian Myles, na mgeni kutoka kutoka Canada, wakishangalia samaki Sato, walipotembelea soko la Mwaloni hivi karibuni. Kushoto ni Ofisa wa CRDB Microfinance Mwanza, Raymond Urassa.
Wafanyakazi wa CRDB Microfinance ya Mwanza, wakitembeza wageni mbalimbali kushuhudia maendeleo ya wafanyabiashara wa Soko la Mwaloni, Kirumba, Mwanza ambao wamefaidika na mikopo ya CRDB Bank inayoratibiwa na kampuni ya CRDB Micrfinance kwa lengo la kuwawezesha wajasiliamali wadogo na wa kati kwa kuwapatia mikopo ya mitaji na kuwafunganisha na fursa za masoko.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...