Baada ya kutangaza Olduvai Gorge na Mlima Kilimanjaro upo kwao, Watani wetu wa Jadi  sasa wamehamia katika kutumia jina la mlima huo mrefu kuliko yote barani Afrika kwenye ndege zao. Tujadili hili. Mdau unazungumziaje hili na maudhi mengine hayo?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 42 mpaka sasa

  1. sisi tumelala,wacha wao watumie wafaidike

    ReplyDelete
  2. naona kuna mahali tunapokosea kuhusu namna ya kuvitunza na kuvienzi vitu vyetu kwa manufaa yetu. Ila kubwa pia kwa kuwa Nairobi kuwa kama ndio kitovu cha kuwashusha au kupitia watalii wengi kwa sisi kutokuwa na shirika la ndege la kuweza kufanya kazi maeneo mbalimbali imekuwa kama advantage kwa KQ Mdau mkubwa na mkombozi wa wengi kwa safar za nje kutumia Mt Kilimanjaro kutangaza biashara yake kwa msingi kuwa ukitaka kutoka west Africa, Europe, America na kwingineko kwenda kuona Mt Kilimanjaro board KQ.
    hivyo hili lina pande mbili za coin

    ReplyDelete
  3. Miss-representation, fraud, deception, etc.
    Kenya government is unethical, it allows this.

    wako radhi kusema uongo ili wapate ile penny.

    sishangai wakisema magufuli amshinda uhuru.

    ReplyDelete
  4. SASA SISI TUMEKAA TU USWAHILI NA KUTUMBUANA MAJIPU WAKATI WENZETU WANAONA MBALI, NA BADO MPAKA WATAKUJA TANGAZA ARUSHA NI KENYA SISI TUMELAA TU VIONGOZI WETU WAMEKALIA USWAHILI TU HAMNA LOLOTE LA KUPIGANIA RASILI MALI ZETU.

    HIO SIO SIRI DUNIA NZIMA WANAJUA MLIMA KILIMANJARO UPO KENYA MPAKA HAPA UK, MAREKANI NDIO USISEME, SASA HATUNA NDEGE HATA MOJA TUTATANGAZA NINI?

    KAMA KWELI MAGUFULI ANA AKILI YA KWENDA SHULE AFUFUE HILO SHIRIKA ILI NA SISI TUANDIKE NGEGE ZETU HIVYO.

    BADO TUMELALA SANA, EWE MUNGU TUFUNGUE MACHO NA SISIS TUWEZE IONA HII DUNIA AMBAYO HATUIONI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hii swala la kutumbuliwa wengi linawaumiza hasa wale waliokuwa wanajiona vigogo. Wanatumia madaraka vibaya kwa wizi,rushwa,ufisadi alafu nchi inabaki tiii na waliowengi ni masikini kiasi yakwamba tutaendeleaje kwa khali hiyo. Wacha watumbuliwe ndio watu watajua wajibu wao. Na wengine wasiowajibika na kazi zao. Kenya iko afadhali zaidi kuliko sisi ilikuwa hasa uongozi uliopita. Ulidolola sana ndio maana tupo tupo tu tungekuwa angalau tumepiga hata hatua mmja lakini WaPi? ni kukwamishana sisi kwa sisi na ni nani? Kigogo inamaana tajiri na nani? Masikini huo utajiri wenyewe sasa rushwa ufisadi wizi urikithiri hata kiasi hakuna ndio maana lii nchi litaendeleaje? Wacha WATUMBULIWE tena kwa herufi kubwa zaidi.

      Delete
  5. Nafikiri serikali ya Tanzania Sasa ichukue hatua kuwasilisha malalamiko yao rasmi. Hivi tuanavyokaa kimya tunazidi kuwanufaisha tu. Maana tunachukulia masikhara tu na kuona kama vitu vya utani kwenye mitandao wakati wenzetu wapo serious.

    ReplyDelete
  6. Watanzania hatuna vipaumbele. Tunakaa kukimbizana na wanasiasa ambao tunazidi kuwapa majina badala ya kufuatilia vitu vyenye tija kwa nchi. Tuna wataalamu wazuri sana wa mambo ya utalii lakini serikali yetu imekalili majina ya watu wa kufanya nao kazi. Tubadirike kama kweli tunataka kujitangaza. lasivyo tusilalamike tuwaache wakenya wendelee kunufaika.

    ReplyDelete
  7. Tanzania tuna majungu sana...i think we should be happy they are doing the marketing for us...tunavyo lakini tumevikalia what do you expect?let someone who knows the potential of it do use it...tunapenda kuka nyuma ya keybord na ku complain while we are not doing anything to change. Mbona Ethiopian airline wanandege zinaitwa Kilimanjaro.Hatuna hata National arline at least kenya wametuenzi

    ReplyDelete
  8. Hakuna kosa lolote hapa ni mikakati ya kibiashara katika kuvutia wateja kutumia ndege yao.

    KLM pia wanatumia jina hili la Mount Kilimanjaro just google and you will see it.

    Ethiopian Airways nao mojawapo ya ndege zao inaitwa TAJ MAHAL kivutio cha utalii kilichopo India.

    ReplyDelete
  9. Pia inawezekana ilo ni jina la hiyo ndege hachilia mbali ndege uwa zina majina ya namba; etc

    ReplyDelete
  10. Hivi taasisi husika inafanya nini?
    Au ndo wanamsubiri mheshimiwa rais JPM awafundishe kazi...its so sad and shame to us that we can't use our things properly...

    ReplyDelete
  11. Hivi taasisi husika inafanya nini?
    Au ndo wanamsubiri mheshimiwa rais JPM awafundishe kazi...its so sad and shame to us that we can't use our things properly...

    ReplyDelete
  12. Ata wakitaka kuitumia lake Victoria acha watumie mwisho wa siku wanatutangaza hawawezi kubeba mlima kupeleka KWAO wala hawawezi kuharisha lake Victoria huko Tunaita kujikomba

    ReplyDelete
  13. JPM akishanunua ndege zetu za ATCL nasi tuandike hivyo na amtake Raisi Kenyate afute mara moja hayo maandishi kwenye ndege zao

    ReplyDelete
  14. Sasa, watasema, JPM, ni raisi, wa Kenya very soon.

    ReplyDelete
  15. Nakubaliana na National Parks Blog, hawa watu wameanza kutumia hayo majina tangu zamani kwa hiyo tusianze leo kupiga kelele. KLM ndege yao ilikuwa na jina la 'Mount Kilimanjaro' kabla hata KQ hawajapata hii ndege. Na kuna wakati KLM waliita B777-300 mojawapo "Serengeti' tena tukafurahia. Sasa kwa nini leo tuwakabe koo hawa KQ sababu ya hili jina? Na sisi tununue za kwetu tuziite majina ya vivutio vyetu.

    ReplyDelete
  16. mimi nionavyo hata wao wana haki kwa sababu mtalii anaweza kuuona mlima akiwa ktk ardhi ya kenya

    ReplyDelete
  17. Hoja za kusema tumelala hazina mashiko. Huwezi kwenda kuchukua mali ya mtu ukaanza kuitumia kwa kisingizio cha kusema nimeona mwenye nayo haitumii. Huo ni wizi. Kama wana akili watumie vya kwao kupata mali. Kutumia cha mtu bila ridhaa yake huo ni wizi. Nafikiri Rais wao yuko sahihi. Wizi ni wizi tu. Tumieni mali zenu na si za wengine....

    ReplyDelete
  18. Hi makubwa

    ReplyDelete
  19. WATANZANIA USHAMBA,MAJUNGU NA UDOKOZI NDIYO MNACHOWEZA HAMNA HATA NDEGE MOJA NCHI AMBAYO INATEGEMEA ASILIMIA KUBWA KATIKA PATO LA TAIFA UTALII WAKATI HAINA HATA TWIN OTTER SHAME ON YOU MKAPA ANAONGOZA KWA KUIUA AIR TANZANIA.VIONGOZI WA TANZANIA WALAANIWE KABISA KWA KUWEKA MBELE KUPIGA DEAL MUNGU WAONYESHE

    ReplyDelete
  20. Jamani hawa watu TTb hawana wanasheria wakawasaidia? jina Kilimanjaro halina hati miliki ya mtu yeyote. Hata Burundi wakitaka kuita ndege yao Kilimanjaro huwezi kuwashutumu. Mbona watu wetu wamelala. sasa maketing gani ya TTB isiyojua sharia za marketing?

    ReplyDelete
  21. Hapa kuna jambo!!Labda ni Franchising na wanatulipa,wakuu watujuze.Au wamefanya au wanatumia Nembo yetu/Ishara yetu na wanalipia ila kwa hili la nembo ya Taifa, ni kuuza utamaduni.Please wakuu watolee maelezo maana its too much now!

    ReplyDelete
  22. Wana wazimu hawa hupenda sana kujisifu na kujin awana akili nyingi kwa mambo ya uongo ,,,,hawana mpango ni wezi tu

    ReplyDelete
  23. Acheni jazba Tanzania friends. Kaa chini and review international laws relevant to international names. Your Tourism Board may want to do some homework before shooting themselves on the foot. A friendly advise from jirani mwema.

    ReplyDelete
  24. Maendeleo hayaji kea kinyongo, vitu vingine ni vyanchi ila virginee ni lasirimali ya Bara zima Hamuwezi kuendelea bila kushirikiana na mataifa mengine haijatokea mtu akajitosheleza kwa kila kitu, Mbona Tanzania kuna the Guradian, Mbona kuna mabazi yenye majina kama Scandinavia etc. Hata tulioko huku majuu Watanzania ni majungu tu, kazi zetu kusengenya wakati wengine wakitafuta riski

    ReplyDelete
  25. Jamani mie hata sioni tatizo liko wapi. Kwani si ndege zao ndio zinawaleta watalii kuuona huo mlima? Kama tuna shida sana na hilo si tuendeshe ya kwetu tuiite Mt. Kenya! tukiita hivyo si watalii wataingia na kulala Arusha tukapada visenti vya kuwaweka kwenye hoteli zetu kisha wakasafiri kwa gharama zaidi kuelekea Kenya kuuona mlima husika?

    ReplyDelete
  26. Ben Toronto.March 02, 2016

    Kenya wamelilipia hilo jina kwa serekali ya Tanzania, Kama ilivyo wahabeshi wanavyoitumia Taj Mahal..Tatizo kwa sisi bongo inawezekana kuna kamchezo kalichezwa na wahusika wakuu, wamekula mkwanja..huenda hili nalo likawa jipu..LITUMBULIWE !!

    ReplyDelete
  27. Magufuli afanye mabadiliko ya jina la mlima kilimanjaro aupe jina jpya na afanye party kubwa sana.

    ReplyDelete
  28. could not agree more. why don't we buy our airbus and Christine or nickname it mt. Kenya?

    ReplyDelete
  29. Watanzania can you be so small? You are truly angry!

    ReplyDelete
  30. Nakubali tununue yakwetu na kuiita mt Kenya. Wenzetu watafurahi tu tunawatangazia mlima wao. Sisi vita. Kweli nchi ya amani na utulivu. Hapa ndio pakupigania?

    ReplyDelete
  31. Tatizo ni kusema mlima uko Kenya. Let them be honests. Kuweka nembo na jina kwenye ndege yao halina shida. Shida inaanza wanapo enda mbali zaidi na kusema mlima uko Kenya. Ni kweli ukiwa Kenya unauona tena vizuri tu. Lakini hauko Kenya. Hata hiyo Oldivai Gorge haiko Kenya. Nimwendelezo wa kujitajia vitu ambavyo haviko nchini mwao.

    ReplyDelete
  32. Wakuu wapo Arusha kuongelea integration wakati TTB wanalilia majina. Ajabu sana. Vipaumbele vipo wapi? Huu ujinga watu wanalipwa kuuonyesha?

    ReplyDelete
  33. Hakuna kosa kwa Jirani zetu kutangaza Mlima Kilimanjaro kama sisi wenyewe hatuna ndege hata moja acha wao watangaze.
    Fahamu huwezi kupanda mlima mpaka uje Tanzania lakini pia TANAPA na wadau wengine wakwetu wamelala ni wakutoa kwenye izo nafasi hawatoshi.
    Kama tukiandaa onyesho kubwa NEWYORK NA KUOMBA NAFASI ya kuweka bango letu katika LIBERTY STATUE pale unapo ingilia tukionyesha kuwa lima Kilimanjaro upo Tanzania itasaidia.
    Wanaongalia TV marekani mpaka kusubili tangazo letu kiukweli inachukua mda sababu matangazo kwao ni engi mno.
    Pia tunaweza kuomba serikali ya wingereza tukaweka matangazo kwenye mabasi yao linalo onyesha mlima Kilimanjaro hivyohivyo hata Japani na China nchi zenye watalii wengi.Kenya tusiwalaumu wanatumia uzembe wa watu wetu.

    ReplyDelete
  34. Inasikitisha hatakama tumelala ndio watuibie? hizi ni dalili zakuishiwa hawana vivutio vya mana i think wametuamsha.

    Hili ni jipu ngoja magufuli alete ndege zake alizo ahidi na cc tutaandika hivyo hivyo halafu tuone wazungu watapendelea kwend nchi gani.

    ReplyDelete
  35. yawezekana wanafuata historia ya zamani kwamba mombasa ilikuwa tanzania na mlima kilimanjaro ilikuwa kenya so wakabadilishana kimaslahi kwakuw kipindi kile mlima kilimanjaro ulikuw hauna ishu lkn bandari ya mombasa ilikuwa na ishu ndo mana kenya wakaamua kubadilishana mlima na bandari kiukweli hapa baba wa taifa aliona mbali

    ReplyDelete
  36. Hakuna haja ya kuwa na jazba. Tuwe na utaratibu wa kusoma kwani kwamba Kilimanjaro ipo wapi lopp wazi kiwa upo Tanzania na ulimwengu wote unajua. Swali ni je tunautumiaje uwepo wake Tanzania kwenye kijenga uchumi wa nchi. See the link below

    https://en.m.wikipedia.org/wiki/Mount_Kilimanjaro

    ReplyDelete
  37. Why even petition a young and historically and geographicaly ignorant young girl like her. That shows how sirious not she is in at least visiting litetature before she utter words. She is proind of nothing she knows.

    ReplyDelete
  38. KLM nayo ina kilimanjaro hawana mahana mlima uko uoranzi

    ReplyDelete
  39. Kwanza wanautangaza kwa kupitia raslimali zao. Mlima uko east Africa. Tatizo lenu mini? Sisi si tumefeli kila nyanja. Mijitu imekali wizi tu. Mpka viongozi usiseme sasa tutaendeleaje. Mtu anapewa kazi yeye anawaza wizi. Mtu anapata kazi ya uongozi anawaza wizi.ufisadi rushwa hamna kingine cha maendeleo bali ni hayo tu. Mfano awamu iliyopita mabilioni ya hela za ufisadi. Wanasema vijihela vya mboga mara visenti. Kweli wahenga walisema kosa mali pata akili.

    ReplyDelete
  40. Hivi haiwezekani kuwashitaki? Nadhani wakati umefika wa kuwashtaki na watulipe fidia.

    ReplyDelete
  41. Hivi mnadhani jina Oysterbay ni la Tanzania? Acheni ujinga. Watu wakiamua kuiita Ndege kubwa kuliko zote duniani Kilimanjaro ama Serengeti tutapiga kelele? Hiyo ni promotion ya bure kwetu. Kwanini tunakuwa wajinga kiasi hiki? Nashanga hili shirika la utalii nalo ni ouzo kiasi hiki. Hawa Ttb kweli wanalipwa kwa ujinga huu. Magufuli majipu Kama haya hayaoni?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...