Mkurugenzi wa ASpro Capital, Isaya Shoki akizungumza na waandishi habari juu ya mkutano wa wajasiriamali na Wafanyabishara wakati utaofanyika Aprili 29 katika Ukumbu Ubungo Plaza leo,jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakimzikiliza Mkurugenzi wa ASPRO Capital, Isaya Shoki leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAJASIRIAMALI  wanashindwa kufikia malengo  kutokana na kukosa maarifa ya uendeshaji biashara zao  hivyo wanahitaji wataalam wa kuwasaidia kwenye  biashara zao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuruegenzi wa Aspro Capital Group, Isaya Shoki amesema kuwa wajasiriamali kutokana na kukosa maalifa na wataalam na mitaji ya uendeshaji wa biashara Aspro Capital Group imeamua kufanya mkutano wa wajasirimali wadogo na wafanyabiashara wa kati katika kutoa elimu juu jinsi ya kuwawezesha na hata kutatua changamoto zao za mitaji,na masoko utakaofanyika Aprili 29 katika ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Plaza.

Shoki amesema kuwa Aspro Capital itaweka mawakala katika kila nchi ambapo wafanyabiashara wanaweza kupata masoko ya biashara zao na kuweza kufikia malengo yao.

Amesema wajasirimali baadhi yao wamekuwa hawana vigezo vya kupata dhamana  kutoka taasisi za fedha kutokana na biashara  zao kukosa michanganuo ya kuweza kupata dhamana hiyo.

Shoki amesema Aspo Capital imeanzisha uwekezaji wa hisa zisizosajiliwa katika kampuni mbalimbali ambapo kwa wajasirimali ni moja ya njia ya kuweza kufikia malengo.

Amesema wajasiriamali wakiweza kupata mifumo ya uendeshaji biashara wanaweza kulipa kodi kuliko kutokana kukosa mifumo hiyo.

Shoki amesema kuwa wataalam wanampango  wa miaka 10 katika kuwekeza katika viwanda vya korosho,matunda ,Ngozi pamoja na Pamba ili nchi iweze kufikia uchumi wa kati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...