Na Bashir Yakub.
Yapo mambo mengi ya kufahamu kuhusu bima za magari. Yako mambo ya sera na sheria. Lakini kubwa yapo mambo yanayohusu hatua za kuchukua pale panapo ajali. Zipo aina nyingi za bima lakini makala yataeleza kuhusu bima za magari. Na hasa bima ya mhusika wa tatu ( third party insurance).
Tunahitaji kujua kwanini magari yakigongana hata iwe kidogo tu kwa pasi watu wazozane. Kwanini ulazimike kumlipa mtu pesa nyingi eti kisa umempiga pasi.
Kwanini mtu akushinikize kumlipa hapohapo kwenye ajali. Kazi ya bima ninini na unachoogopa ninini mpaka ulazimike kumlipa mtu hela nyingi tena kwa unyonge mkubwa. Haya yote tutaona.
1.USIMLIPE MTU HELA.
Inapotokea ajali iwe zile ajali kubwa au ndogo maarufu kama pasi awali ya yote tunahitaji kujua nani kati ya madereva wawili ana wajibu wa kutoa taarifa kwa kampuni ya bima husika. Kujua nani anapaswa kutoa taarifa tunahitaji kujua nani aliyemgonga mwenzake.
Kimsingi yule aliyemgonga mwenzake ndiye anapaswa kutoa taarifa kwa kampuni ya bima husika. Kama ni wewe umesababisha ajali basi yafaa utoe taarifa kwenye kampuni yako ya bima.
Hii ni kwasababu ikiwa wewe ndio uliyegonga gari jingine basi kampuni yako ndiyo itakayotakiwa kulipia ile hasara na sio wewe. Kwahiyo kutoa kwako taarifa ni kujiondoa katika dhima(liability) ya kutakiwa kulipa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...