Ni vyema tukakumbushana kwa ndugu zetu Madereva,wanapaswa kuwa makini muda wote wawapo barabarani,uzembe kidogo unaweza ukagharimu hasara kubwa ikiwemo upotevu wa maisha ya watu na mali zao.Mfano wa madereva hawa wa Dala dala hizi kama zionekanavyo pichani,huu ni uzembe mkubwa na uvunjaji wa sheria za barabarani wa makusudi ka.Jeshi la Polisi liendelee kuchukua hatua kali kwa madereva wa aina hii.
Picha hizi zimenaswa mapema leo katika barabara ya Mwai Kibaki rodi na mpiga picha wa Globu ya Jamii aliyekuwa kwenye shughuli zake za kikazi.





Bwana Michuzi, kazi nzuri. Hawa madereva wanaua watu kila siku.police hapa wanauthibitisho wa kutosha. Wasisubiri mpaka watu wapoteze maisha ndio waanze kuwafuatilia hawa madereva na wenye magari.wanaomiliki haya magari pia wanatakiwa wawachukulie madereva adhabu ikiwezekana hata kuwanyang'anya magari. Mbona madereva wako wengi tu wanaotafuta kazi. Pia ningeshauri kama ikiwezekana bwana michuzi uamzishe kona ya usalama kwenye blog yako na uhamasishe watu wakutumie picha za matukio ya barabarani.Na ikiwezekana police wawe wanafuatilia hii kona kuangalia madereva sugu ili wachukuliwe hatua staiki.
ReplyDeleteMdau Edmonton