Ripota wa Globu ya Jamii Sultani Kipingo leo katembelea Daraja jipya la Kigamboni ambalo na kukuta limegeuka kivutio kikubwa cha watalii wa ndani, ambapo mamia ya wananchi kutoka sehemu mbalimbali za jiji na hata mikoani wamejazana darajani hapo kwa mamia kujionea suluhisho la tatizo la usafiri kwa wanaokwenda na kutoka wilaya mpya ya Kigamboni, mkoa wa Dar es salaam. 
Daraja hili lenye urefu wa mita 680 na amblo limeanza kujengwa mwaka 2012 linamilikiwa na mfuko wa jamii wa NSSF kwa asilimia 60 na Serikali asilimia 40. 
Ujenzi wake umeenda sambamba na ujenzi wa barabara ya kilomita 5.7  na gharama yake ni  kiasi cha Dola za Marekani 143.5, ambapo serikali imetoa asilimia 40, huku NSSF ikitoa asilimia 60 ya fedha zote. Designer wake ni Arab Consulting Engineers na wajenzi ni China Railway Jiangchang Engineering (T) Ltd & China Major Bridge Engineering Company.
 Familia ikipita njia ya waendao kwa miguu katika daraja la Kigamboni leo
 Mamia ya watalii wa ndani wametembelea daraja hilo ambalo lilifunguliwa Jumamosi kuruhusu wananchi wajionee, kabla ya kuanza kazi baada ya kufunguliwa rasmi Jumanne hii
 Wananchi wakifurahia daraja la Kigamboni leo
Taswira ya daraja la Kigamboni kutoka angani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hongera wahusika kwa kazi nzuri angalau limekwisha.Hivi ulinzi wa daraja upoje? Maana wasije vibaka wakawa wanavizia watu na kuwakaba wakikutishia kukutupa baharini.

    ReplyDelete
  2. Nchi yazidi kuendelea mbele. Sasa kigamboni itapanuka kuwa pekee city nyingine.Congratulations.

    ReplyDelete
  3. HONGERENI NSSF KWA KAZI NZURI, ILA KWA UPANDE WA KIGAMBONI BARABARA UNGANISHI (ACCESS ROADS) MMEZISAHAU NA HIVYO KUTIA DOSARI KAZI NZURI MLIYOFANYA

    ReplyDelete
  4. Ili kudhibiti masuala ya wizi watu wakaguliwe, pia wasikae ovyo darajani maaskari wafanye patrol, vinginevyo eneo hilo litageuka kitega uchumi kwa kuwatisha wengine au kuwaibia hapo darajani. Hebu mamlaka myafaniege kazi maoni yanayotolewa na wadau!

    ReplyDelete
  5. HONGERA SANA JK KWA KAZI NZURI.

    ReplyDelete
  6. Uchafu uchafu ndiyo jadi yetu./ with no time utaona matakataka yataanza kutupw wamachinga wataanza kuuza bidhaa. Naomba wamachinga iwe maruku huko.

    ReplyDelete
  7. This is something else, congratulations to us all.Sasa hii ni nchi mpya kwangu.
    Nangojea kwa hamu kuja kuiona Bongo ilivyobadilika.
    Nilipoondoka taxi tangu Muhimbili mpaka uwanja wa ndege nililipa shilingi ishirini.

    ReplyDelete
  8. Mdau ulieondoka nchini muda mrefu, hakikisha ticket yako ina muda wa kutosha maana hutatamani kuondoka haraka. Sio tanzania ulioiacha................

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...