Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mh. Ally Salum Hapi jana tarehe 26/4/2015 alifanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoko manispaa ya Kinondoni. Katika ziara hiyo ambayo aliambatana na watendaji mbalimbali wa Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni, Mh. Hapi alikagua na kupokea taarifa ya miradi mbalimbali iliyokamilika na inayoendelea kukamilika. Miradi iliyotembelewa ni kama vile
-Mradi wa ujenzi wa soko la kisasa Mburahati utakaogharimu Bilioni 1.8,
-Mradi wa ujenzi wa barabara ya Arsenal Magoti uliogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 1,
-Mradi wa ujenzi wa wodi ya wazazi Ubungo uliogharimu shilingi milioni 50,
-Ujenzi wa hostel ya wasichana katika shule ya sekondari Mabwepande utakaogharimu shilingi 283,988,270,
-Mradi wa ujenzi wa barabara ya Arsenal Magoti uliogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 1,
-Mradi wa ujenzi wa wodi ya wazazi Ubungo uliogharimu shilingi milioni 50,
-Ujenzi wa hostel ya wasichana katika shule ya sekondari Mabwepande utakaogharimu shilingi 283,988,270,
-Ujenzi wa Kalavati Mabwepande utakaogharimu shilingi 320,880,400,-Ujenzi wa Kituo cha Kilimo Malolo Mabwepande utakaogharimu shilingi 96,412,200 na-Ujenzi wa kisima cha maji Makongo utakaogharimu shilingi 240,000,000.
Akiwa katika mradi wa Kilimo Mabwepande, Mh. Mkuu wa Wilaya alivutiwa na mradi huo ambao unalenga kuweka programu ya kuwafundisha wananchi kulima mbogamboga, kufuga kuku, samaki na ng'ombe. Mh. Hapi alitoa agizo kwa Mkurugenzi kuhakikisha fedha zilizosalia kulipwa mkandarasi kiasi cha shilingi milioni 30 zilipwe haraka ili kituo kikamilike, jambo ambalo lilikubaliwa palepale.
Miradi ya maendeleo iliyokaguliwa inatarajiwa kuzinduliwa na mwenge wa uhuru ambao unatarajiwa kuwa Kinondoni katikati ya mwezi ujao.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mh . Ally Salum Hapi akielekezwa jambo alipokuwa akikagua moja ya mradi ndani ya wilaya hiyo.
Mh. Hapi akikagua na kupokea taarifa ya miradi mbalimbali iliyokamilika na inayoendelea kukamilika.
Mh. Hapi akipata maeelezo mara baada ya kagua na kupokea taarifa ya miradi mbalimbali iliyokamilika na inayoendelea kukamilika.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...