Jumla ya watoto 120 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza, kufuatia tatizo la kichwa kikubwa walilozaliwa nalo chini ya udhamini wa taasisi ya GSM ambayo imedhamini zoezi hilo litakalofanyika katika mikoa mitano ikiwa ni awamu ya kwanza kati ya nne zinazotarajiwa kufanyika tanzania nzima.

Akiongea na waandishi wa habari katika uzinduzi wa zoezi hilo linalojumuisha madaktari Bingwa 10 kutoka Taasisi ya mifupa na Upasuaji MOI, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Profesa Kien Mteta aliishukuru taasisi ya GSM kwa kuamua kulichukua tatizo hilo ambalo ameliita kuwa ni kubwa ukilinganisha na jinsi linavyochukuliwa na jamii ya watanzania.

Dk Kien aliwaambia wanahabari kwamba jumla ya watoto 2000 huzaliwa na vichwa vikubwa katika kanda ya Ziwa peke yake, na mtaalamu wa kuhudumia wagonjwa wa namna hii ni mmoja tu ambapo pia kwa Tanzania nzima, wataalamu wa upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa wako tisa tu.

Cha kusikitisha ni kwamba kati ya hao, ni wachache sana hurudi kwa ajili ya matibabu bali wengi wao hufariki kwa kufichwa ndani na wazazi wao aidha kwa imani za kishirikina ama kushindwa kwa wazazi kumudu gharama za matibabu.
Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Profesa Kien Mteta (kulia) akiongea na wanahabari huku akisikilizwa kwa umakini na Mkurugenzi wa taasisi ya Mifupa na upasuaji Dk Othman Kiloloma (katikati) pamoja na Mkuu wa mawasiliano wa Taasisi ya GSM, Halfan Kiwamba.
Mtaalamu wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya Fahamu, Dk Gerald Mayaya akitoa ufafanuzi kwa wanahabari kuhusiana na kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa katika Hospitali ya Bugando.
Meneja Mkuu wa taasisi ya GSM, Shannon Kiwamba (katikati) akiongea na wanahabari kuhusiana na sera yao mpya ya kusaidia watanzania katika masuala ya elimu na Afya, kulia kwake ni Mkuu wa Hospitali ya Bingando, Prof Kien Mtena na kushoto kwake ni Mkuu wa mawasiliano wa Taasisi ya GSM, Halfan Kiwamba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...