Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio (mwenye miwani ya jua) akikabidhi mfano wa hundi ya Tsh. 150,000,000/ kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego , Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bi. Fatma Ally, Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia na viongozi wengine wa Halmashauri wa Wilaya ya Mtwara.
---------------------------------
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limelipa tozo ya kwanza ya huduma (Service Levy) inayotokana na shughuli za kuzalisha, kuchakata na kusafirisha gesi asilia kutoka Madimba hadi Dar es Salaam. 
TPDC imelipa kiasi cha Tshs. 150,000,000 ikiwa ni tozo ya huduma kwa shughuli za kuzalisha, kuchakata na kusafirisha gesi kuanzia mwezi Oktoba 2015 hadi Machi 2016 (miezi sita). Kiasi hiki kinajumuisha pia fedha kutoka Kampuni ya Maurel and Prom Tanzania Ltd ambayo ni wazalishaji wa gesi katika kitalu cha Mnazi Bay kilichopo kijiji cha Msimbati, Mtwara.
Akiongea wakati wa kukabidhi mfano wa hundi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio alisema malipo ya tozo ya huduma yatakua yakifanywa kwa kipindi cha miezi mitatu mitatu ili kuwezesha Halmashauri kutekeleza mipango yao ya maendeleo bila kukwama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tozo hii itumike vizuri kuleta maendeleo katika sehemu husika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...