Jumla ya dola milioni 20 za Marekani zimetumika kwa ajili ya kutengeza kiwanda kipya cha vinywaji vikali maarufu kama nyati spirit Tanzania .
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mkuu wa uhakiki wa kiwanda hicho Karan Suchak amesema kuwa pamoja na kuingia katika soko la ushindani la vinjwaji vikali pia ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ambapo watanzania zaidi ya mia moja wamepata ajira huku idadi yao ikitarajiwa kuongezeka.
Kwa upande wa afisa habari wa kampuni hiyo Alma Miraji amesema kuwa vinywaji hivyo havitakuwa na madhara kwa mtumiaji kutokana na kuthibishwa na shirika la viwango Tanzania (TBS) pamoja na mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) huku wakikusudia kuweka nembo maalumu itayotenganisha na bidhaa nyingine feki.
Alma ameongeza kuwa vinywaji ambavyo vinapatikana kwa ladha tofauti ikiwemo kahawa matunda havitoruhusiwa kutumiwa na watoto walio chini ya umri wa miaka 18 kutokana na kuwa na kilevi kama ilivyo vinywaji vingine.
Afisa
Habari wa kampuni ya nyati Spirit Tanzania,Alma Miraji akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya vinywaji vya kiwanda cha
Nyati Spirit Tanzania havitakuwa madhara kwa mtumiaji kutokana na
kuthibishwa na shirika la viwango Tanzania (TBS) pamoja na mamlaka ya
chakula na dawa (TFDA) leo jijini Dar es Salaam kuliani Mkuu wa uhakiki
wa kiwanda hicho Karan Suchak.
Wafanyakazi
wa kiwanda cha Nyati Spirit Tanzania wakitoa maelekezo juu ya kutotumia
watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane kutokana na kuwa na
kilevi kama ilivyo vinywaji vingine vikali .
Wafanyakazi wakiwanda hocho wakipanga vinywaji katika mabosi .(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii)
The mdudu, to be honest mimi viwanda vya kuuwa watanzania si viungi mkono mbona hamjengi viwanda vya nguo? au vya kusindika matunda coz Tanzania yetu imejaliwa na neema ya matunda ya kila aina
ReplyDeleteAudhubillah
ReplyDeleteMwajenga viwanja vya kututengenezea sumu ya mwili na utu
Ningefurahi sana kama kiwanja hicho kingekuwa ni cha kutengeneza madawa,chakula etc even mbolea but not vinywaji, tena vikali.
Masikini kila siku anadhulumiwa, kwani kuniwekea sumu ili nijiue kwa ujinga wangu ama matatizo yangu ya maisha ni dhuluma.
I know its not illegal but I think its immoral.