Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria, (B) Mohamed Chande Othman akiwa na Makamu wake pindi walitembelea ofisini kwa Mhe. Jaji Mkuu mapema leo. Lengo likiwa ni kujitambulisha na kupata maelezo mafupi juu ya Mahakama ya Tanzania.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria wakiwa katika mazungumzo na Mhe. Jaji Mkuu mapema leo walipotembelea ofisini kwake kwa ajili ya kujtambulisha na kupata maelezo mafupi ‘brief notes’ juu ya Mahakama ya Tanzania. 
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman akimkaribisha mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama walipotembelea ofisini kwake mapema leo.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati wakimsikiliza Jaji Mkuu (hayupo pichani) mapema leo walipozuru ofisini kwake. Pamoja na mambo mengi Mhe. Jaji Mkuu amewaeleza wajumbe hao kuwa Mahakama ya Tanzania ipo katika maboresho mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumaliza kesi za muda mrefu Mahakamani. 
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...