Na Bashir Yakub.
Kutoa ushahidi wa uongo ni kosa. Ni kosa lenye adhabu kisheria. Ushahidi wa uongo ni pamoja na kupanga au kupangiwa la kusema mahakamani wakati mkijua kuwa sio la kweli.
Kosa hili ni moja ya makosa yanayotendwa mno tena kiholela. Ni kawaida watu kupanga waseme nini mahakamani huku wakijua wanachopanga sio cha kweli.
Suala la ushahidi wa uongo halijalishi kesi ni ya aina gani. Iwe jinai au madai shahidi anawajibika kuwa mkweli daima.
Kisichotakiwa ni kusema uongo ambao hupotosha usimamizi bora wa haki.
1.NAMNA YA KUWACHUKULIA HATUA SHAHIDI WAONGO.
Ni wajibu wa mtu wa upande wa pili katika kesi kuchukua hatua dhidi ya shahidi msema uongo. Ikiwa uko upande wa pili wa kesi na shahidi wa upande mwingine anatoa ushahidi wa uongo dhidi yako ni wajibu kwako kuchukua hatua haraka sana.
Hatua inayofaa ni hii ya kutoa taarifa polisi au kwa hakimu/jaji husika ili kumfungulia mashtaka shahidi kwa kusema uongo.
2. KOSA LA KUTOA USHAHIDI WA UONGO KATIKA SHERIA.
Kifungu cha 102 cha Kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu yeyote wakati wa kufungua shauri au wakati shauri likiendelea, kwa kujua akatoa ushahidi wa uongo kuhusu suala lolote katika kesi atakuwa ametenda kosa.
Hiki ndicho kifungu cha sheria kinacholitangaza tendo la kutoa ushahidi wa uongo kuwa kosa( perjury).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...