Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akishuhudia mabati yaliyotolewa ma Mfuko wa Pensheni LAPF kwa ajili ya ujenzi wa madarasa wilayani Geita ikiwa jitihada za Mfuko wa LAPF kuunga mkono jitihada za Serikali kutoa elimu bure. Jumla ya mabati 300 yenye thamani ya Shs. 7,000,000/= yalikabidhiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akikagua mabati yaliyokabidhiwa kama msaada na mfuko wa Pensheni wa LAPF wilayani Geita, kulia ni Meneja Masoko wa Mfuko wa LAPF Bw. James Mlowe wengine ni maofisa kutoka wilaya ya Geita.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita akitoa neno la shikrani kwa Mfuko wa Pensheni LAPF kwa msaada wa mabati 300 yanayotosheleza kuezeka vyumba sita (6) vya madarasa yanayoweza kuchukua wanafunzi 45 kwa kila chumba na hivyo kupunguza tatizo la ukosefu wa mazingira bora ya kufundishia.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akiteta jambo na Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni LAPF James Mlowe pamoja na wafanyakazi mbalimbali wa Wilaya ya Geita mara baada ya makabidhiano ya msaada wa mabati kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...