leo
(JANA) 31/03/2016 Mkuu wa wilaya Iringa ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa
ameshiriki kwenye mazishi mazishi ya Mnywarwanda Jeannnete Mukashema
aliyefariki kwenye ajali iliyotokea usiku Juzi. Bi Jeanette alikuwa
akisafiri na mtoto wake ambaye naye aliumia kwenye ajali hiyo bado
anaendelea na matibabu.
Akizungumza Mh Kasesela alisema " Imeniuma sana
kwani niliupokea mwili kwa mikono yangu tukiwa na waokoaji wengine alipo
tolewa juu kwenye basi bado tukio hilo limo mawazoni mwangu na nguo
zangu zikiwa na madoa ya damu , tulimpokea akiwa tayari amefariki.
Kesho
yake mtoto alipo zinduka akaanza kumtafuta mama yake nilipo mtembelea
asubuhi, nilijua mama yake amekufa nilishindwa kumwambia leo alipo niona
ameanza kulia amenikumbusha nikiwa miaka 11 nilipo ondokewa na mama
yangu. lakini naamini yuko katika mikono salama, Mungu ni mwema baba
yake na ndugu wengine wamekuj kutoka Rwanda. BWANA AMETOA BWANA AMETWAA
JINA LA BWANA LIHIMIDIWE"


RIP Mama, poleni kwa familia hiyo, Kijana tunakuombea Mungu atakulinda. Richard Kasesera, you are such a great leader.
ReplyDeleteJoshefu dar